Kyagwali wanasemaje kuhusu siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake?

Wanafunzi nchini Sudan Kusini wakigiza suala la ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo.
UNMISS/Isaac Billy
Wanafunzi nchini Sudan Kusini wakigiza suala la ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo.

Kyagwali wanasemaje kuhusu siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake?

Wanawake

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana zinaendelea kuadhimishwa kote duniani.  

Ni ukatili ambao Umoja wa Mataifa unasema sio tu unaathiri mamilioni ya kundi hilo na kukiuka haki zao za binadamu bali pia unaacha jeraha lisilokwisha katika akili na maisha ya wanawake na wasichana duniani. Sasa Umoja huo unahimiza nchi zote, mashirika, asasi za kiraia na wadau kuhakikisha wanapambana kwa kila njia kutokomeza jinamizi hili kwani ni chini ya asilimia 10 ya wanawake na wasicha wanaoathirika ndio wanaouripoti. Nchini Uganda mwandishi wetu John Kibego amekwenda kwenye makazi ya wakimbizi ya Kiangwali ambako kampeni zinaendelea ili kubaini je ukatili huo upo? hali ikoje? Na nini kinafanyika kuukomesha? Ungana naye.