Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa UN Women M4C wawapiga jeki wanawake wachuuzi wa visiwa vya Pasifiki

Watoto wakipokea mlo kutoka kwa mwanamke nchini Ecuador
Jamie Martin/World Bank
Watoto wakipokea mlo kutoka kwa mwanamke nchini Ecuador

Mradi wa UN Women M4C wawapiga jeki wanawake wachuuzi wa visiwa vya Pasifiki

Wanawake

Katika visiwa vya Pacifiki kati ya asilimia 75 hadi 90 ya wachuuzi sokoni ni wanawake na kwa kutambua umuhimu wao na mchango wao katika jamii  shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women liliamua kuanzisha mradi wa masoko kwa kwa ajili ya mabadiliko au M4C kwa ajili ya kuwawezesha wanawake hao na familia zao. 

Mradi huo wa M4C unaofadhiliwa na serikali ya Australia , Canada na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP unajikita katika mambo makuu manne  ambayo yanawasaidia wanawake hao kutoyumba katika biashara zao, mosi ni kuwa na jumuiya za wanawake wachuuzi wa sokoni, pili kuwa na uhakika wa usalama wa kijamii na kiuchumi, tatu kuhakikisha kunakuwa na wawakilishi wa serikali wanaozingatia masuala ya kijinsia , uwajibikaji na maslahi yao na nne kuboresha mioundombinu na maandalizi dhidi ya majanga ili kuendelea na shughuli zao.

Haha hiyo safari haikuwa rahisi kwani wanawake hao hawakuwa na sauti kabisa katika biashara zao, haki zao n ahata vipato vyao na wengi walishindwa kutetea maslahi yao kabla ya kuanza kwa mraddi huo, Shobna Verma amekuwa mchuuzi sokoni kwa miaka 27 na sasa ni mshauri wa kisheria wa jumuiya ya SUVA ya wanawake wachuuzi wa sokoni kisiwani Fiji, “Nililazimika kuwa mchuuzi wa sokoni kutokana na mazingira yaliyonisibu , baba yangu kufa . Maoni yetu hayakuwa yanasikilizwa  na tulikuwa haturuhusiwi hata kuokngea na mkuu wa soko   “

Shobna mwenye watoto wawili hakuwa na chaguo likingine la kuhudumia familia yake n ani hali iliyowasibu wanawake wengi kisiawani Fiji.

Katika kisiwa cha jirani cha Vanuatu gharama za kupata fursa ya kuwa na meza ya kuuza sokoni zilikuwa juu sana na hata kusababisha wanawake wengine kushindwa kukidhi mahitaji ya familia zao kama Helen Philemon, “Nilikuwa nauza bidhaa lakini fedha zote zilikuwa zinatumika kulipia meza , sehemu ninanoyouzia, maliwato na kuoga.   Na kama nisipolipa siwezi kutumia meza, nilikuwa naenda nyumbani wakati mwingine bila chochote.

Wanawake hawa wachuuzi visiwa vya Pacifiki walijihisi hawana uwezo wowote wa kubadili mtazamo huo sokoni hadi pale mradi wa UN women wa M4C ulipowasaidia kubadili hali hiyo kwa kuwa sehemu ya kufanya maamuzi miongoni mwao ni Catherine Leo  meneja wa soko la Luganville Vanuatu, "na umesaidia wanawake wengi kusimama kidete kama wachuuzi sokoni, wanatoka katika maeneo mbalimbali na hivi sasa bni wanawake viongozi katika jamii zao na familia zao. “

Hivi sasa mamia ya wanawake wachuuzi Pacifiki wanafurahia sio tu kuuza sokoni bali kukidhi mahitaji ya familia zao na jamii kwa ujumla, wakisema  asante UN Women.