UN yatekeleza kwa vitendo uwezeshaji vijana Tanzania

Kijana kutoka Tanzania na bango la lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalotaka usawa wa kijinsia.
Warren Bright/UNFPA Tanzania
Kijana kutoka Tanzania na bango la lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalotaka usawa wa kijinsia.

UN yatekeleza kwa vitendo uwezeshaji vijana Tanzania

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kauli ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha kuwa vijana wanajengewa  uwezo ili washiriki kikamilifu katika kufanikisha maendeleo endelevu, SDGs imeendelea kutekelezwa maeneo mbambali ambapo nchini Tanzania vijana takriban 50 kutoka wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam, wamepokea mafunzo kwa ajili ya kuimarisha stadi zao za ujasiriamali. 

Mafunzo ambayo yamefanyika chini ya uratibu wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam, UNIC  ambapo akizungumza katika mahojiano maalum na Stella Vuzo, afisa wa habari wa kituo hicho, mkufunzi Lawrence Ambokine amesema,“Tumewafunza kuhusu kubuni biashara kwa hiyo mwisho wa siku kila kijana ameondoka na wazo lake la biashara ambalo litamsaidia kuweza kujua ni biashara ipi ataifanya na aifanye kwa ubora zaidi, tumekuwa na mafunzo mazuri na washiriki wameyafurahia kwa sababu wengi walikuwa wanafanya biashara kwa mazoea lakini sasa wamepitia hatua nne ikiwemo kubuni, kujua sifa za mjasiriamali na kuwa na wazo moja sahihi la biashara.”

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo amesema, “Tumekuja kwenye semina hii kwa nia ya kujifunza namna ya kuanzisha biashara na namna ya kufanikisha biashara hizo na wametujengea uwezo katika kujiamini katika utekelezaji wa biashara.