Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatutochoka hadi mabomu yote ya kutegwa ardhini yateguliwe Sudan Kusini:UNMISS

UNMAS wakitegua mabomu katika eneo la Equatoria mashariki nchini Sudan Kusini
UNMISS\Nektarios Markogiannis
UNMAS wakitegua mabomu katika eneo la Equatoria mashariki nchini Sudan Kusini

Hatutochoka hadi mabomu yote ya kutegwa ardhini yateguliwe Sudan Kusini:UNMISS

Amani na Usalama

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya huduma za kutegua mabomu ya kutengwa ardhini UNMAS, mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan kusini UNMISS na serikali ya Japani wamesema hawatopumzika hadi pale mabomu yote ya kutengwa ardhini nchini sudan kusini  yatakapoteguliwa. 

Katika Kijiji cha Amee jimboni Totit ambako awali iliishi jamii iliyoshamiri ya wakulima wa chakula kama mahindi, maharage, mabiringanya na mazao mengine mengi sasa mashamba yote yametelekezwa kutokana na mabomu ya kutegwa ardhinini yaliyosababishwa na vita vinavyoendelea Sudan Kusini na kuwafanya maelfu ya wakulima kufungasha virago kwenda kusaka maeneo ya kilimo kwingineko. Tobiolo Alberio Oromo ni Gavana wa Torit anasema nchi yake imeaathirika vibaya na vita na pia, "mabomu ya kutegwa ardhini na vilipuzi vingine vimetapakaa nchi nzima, sasa imekuwa shida kubwa kwetu kutumia ardhi."

Hata hivyo leo hii  mahali hapa kuna kila  sababu ya kurerehekea kwani juhudi za kurejesha ardhi hiyo katika matumizi yake ya awali zinaendelea baada ya ziara ya ujumbe wa UNMAS, UNMISS na serikali ya Japan kutegua mambo ya ardhini na kushuhudia hatua zilizopigwa kuelekea 2023 wa kulifanya taifa hilo kuwa huru bila mabomu ya kutengwa ardhini. Richard Boulter ni afisa wa UNMAS anasema,“Tunashukuru sana kwa msaada wa Japan kwa kusafisha na kutusaidia kufanyakazi na mamlaka ya taifa ya kutegua mambo ya kutengwa ardhini ili kuijengea uwezo serikali ya Sudan Kusini.”

Hadi sasa mabomu yameteguliwa katika maeneo 263 na mengine 10 zaidi yanafanyiwa kazi likiwemo eneo la ekari 20 za kijiji cha Amee na zoezi llikitarajiwa kukamilika juni mwakani.

Karibu wanakijiji 25,000 wa Amee wanausubiri kwa hamu kubwa wakati huo. Mkuu wa UNMISS ni David Shearer, “Tunatumai kuendelea na mchakato huu ili Sudan kusini iwe huru kabisa bila mambomu ya kutegwa ardhini, na ili kila mtu aweze kutembea kwa usalama na kuendelea na maisha yao ya kilimo na mengine wanayotaka kufanya katika maisha yao.”