Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watoto milioni 7 duniani wananyimwa uhuru :OHCHR

Issaa mhamiaji kutoka Niger mwenye umri wa miaka 14 akiwa kizuizini nchini Libya Januari 2017. Alikamatwa wakati akijaribu kupanda boti kuelekea Italia.
© UNICEF/UN052682/Romenzi
Issaa mhamiaji kutoka Niger mwenye umri wa miaka 14 akiwa kizuizini nchini Libya Januari 2017. Alikamatwa wakati akijaribu kupanda boti kuelekea Italia.

Zaidi ya watoto milioni 7 duniani wananyimwa uhuru :OHCHR

Haki za binadamu

Zaidi ya watoto milioni 7 kote duniani wanakabiliwa na aina mbalimbali za mateso katika vituo mbalimbali maalumu ikiwemo vituo vya mahabusu vya uhamiaji, vituo vya polisi, magereza na maeneo mengine ya mahabusu.

Hayo ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti yaliyotolewa leo na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, (OHCHR) mjini Geneva, Uswisi ikiongeza kuwa ni bayana kwamba hali hiyo inakwenda kinyume na matakwa ya mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto (CRC) ambao unaeleza kwamba “uwekaji mahabusu watoto uwe tu kama suluhu ya mwisho kwa kwa kipindi kifupi cha muda wa unaostahili.Hii inamaanisha kwamba watoto kimsingi watoto hawastahili kuwekwa rumande  na serikali zinapaswa kila wakati kyafuta kwanza mbinu mbadala badala ya kuwasweka rumande au kuwatupa magereza watoto.”

Wakati kuna baadhi ya hatua zilizopigwa katika miaka ya karibuni, utafiti huo unaainisha haja ya ya kuongeza juhudu za kutowaweka watoto katika vituo vya kushikiliwa , kutafuta suluhu mbadala, kukomesha mahabusu kwa watoto zinazohusiana na masuala ya uhamiaji, na hatua zingine ili kwenda sanjari na mkataba wa haki za mtoto.

Ofisi ya haki za binadamu inasisitiza kwamba utotoni ndio wakati ambapo watoto hao wanajenga tabia zao, mahusiano yao ya kihisia na wenzao, ujuzi wao wa kijamii na kielimu n atalanta zao.

Ni dhahiri kutokana na maoni yaliyotolewa na watoto katika utafiti huo kwamba “kwa upande wao kunyimwa uhuru muhimu inamaanisha kupokonywa utoto wao.” 

Kutokana na mtazamo huo utafiti huo wa kimataifa umesema kwamba kuwanyima watoto uhuru wao ni mfumo wa ukatili wa kitaasisi ambao nchi ziliahidi kuukomesha kupitia lengo la maendeleo endelevu nambari 16 kipengele cha .2, umesisitiza utafiti huo na kwamba “jamii zetu zinaonekana kusahau ukweli mmoja rahisi na muhimu:watoto hawapaswi kushikiliwa mahabusu kwa sababu kuwanyima uhuru inamaanisha ni kuwanyima haki , uharaka, maono, fursa na upendo” amesema Manfred Nowark mmoja wa waandishi wa ripoti ya utafiti huo.