Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa usafiri unahitaji kuwajumuisha wote ikiwemo wanoishi na ulemavu-UN-HABITAT

Wasafiri kwenye basi la mwendo kasi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
UN-Habitat/Julius Mwelu
Wasafiri kwenye basi la mwendo kasi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Mfumo wa usafiri unahitaji kuwajumuisha wote ikiwemo wanoishi na ulemavu-UN-HABITAT

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la makazi la Umoja wa Mataifa, UN-Habitat kwa ushirikiano na taasisi za usafiri na utungaji sera na kamisheni ya kitaifa ya usawa wa kijinsia nchini Kenya wanashirikiana katika kukarabati mfumo wa usafiri jumuishi ambao utawezesha huduma za usafiri kwa watu ambao wanaishi na ulemavu. 

Hatua hiyo inazingatia ripoti ya kwamba licha ya ukuaji kwa kasi kubwa ya miji barani Afrika bado mifumo ya usafiri wa umma inakabiliwa na msongamano, huku ikiwa si ya kuaminika , ya gharama ya juu na isiyo rafiki na salama kwa  wanawake na watu wanoishi na ulemavu.

Kufuatia mikutano mbali mbali na wadau ikiwemo vikundi vya wanawake na vya watu wanoishi na ulemavu, imeelezwa sasa kuwa kuna umuhimu wa kuweka mfumo jumuishi na njia za watembea kwa miguu kwa ajili ya mahitaji ya wote ambapo kwa sasa baadhi ya watu wanatengwa kama anavyosema binti huyu anayetumia kitimwendo

(SAUTI YA binti)

Kwa upande wa Tanzania mfumo wa mabasi ya mwendo kasi ambao umekuwepo tangu mwaka 2016 ni mfano bora kuhusu mipango kwa ajili ya mfumo wa usafiri wa umma katika ukanda wa Afrika  huku ukizingatia mahitaji pia ya watu wanoishi na ulemavu kama anavyosema Abdulazizi Shambe, mwanachama wa chama cha watu walioumia uti wa mgongo nchini Tanzania.

(Sauti ya Abdulaziz)

Kwa upande wake Kiongo Itambu, mratibu wa chama cha maendeleo ya vijana wasioona anasema

(Sauti ya Kiongo)