UPU kupanua wigo wa huduma za kifedha mtandaoni
UPU kupanua wigo wa huduma za kifedha mtandaoni
Shirika la posta duniani, UPU, litazindua huduma mpya ya utumaji fedha kidijitali kwa kutumia mashirika ya posta katika nchi 8 duniani.
Taarifa ya UPU iliyotolewa leo kwenye mji mkuu wa Uswisi, Berne, imemnukuu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Bishar A. Hussein akisema kuwa mradi huo wa usaidizi wa kiufundi katika ujumuishaji wa jamii kwenye huduma za fedha kimtandao, FITAF utatekelezwa kwa kushirikiana na mashirika ya posta katika nchi 8 duniani.
Akifafanau mradi huo, Bwana Hussein amesema, “mtandao mkubwa wa posta tayari umekuwa injini ya ujumuishaji jami katika huduma za fedha kitamdano lakini bado una uwezo wa kufikia watu wengi zaidi wasio na akaunti za benki kupitia mitandao ya kidijitali.”
Amesema FITAF tayari imesaidia kuziba pengo hilo katika mataifa yaliyonufaika na mradi wa awali na sasa utafanya vivyo hivyo katika mataifa hayo manane ambayo ni Burkina Faso, Misri, Grenada, Kyrgyzstan, Mongolia, Morocco, Nigeria, na Tunisia.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, watu wazima bilioni 1.7 duniani kote bado hawana huduma rasmi za fedha ambapo sasa kupitia ofisi zaidi ya 600,000 za posta kote duniani, kupitishwa kwa huduma za kisasa za kifedha kupitia mtandao wa posta kunaweza kuwa jibu mujarabu kwa ujumuishwa wa fedha.
UPU inaseam tayari watu bilioni 2 wananufaika na huduma hiyo ya ujumuishwa wa fedha kupitia mtandao wa posta.
Mradi huo FITAF wa UPUkwa ubia na taasisi ya Bill na Melinda Gates na kampuni ya Visa unalenga kusongesha ujumuishwa wa fedha kimtandao kwa na utapatia mashirika ya posta usaidizi wa kiufundi ili waweze kutoa huduma hizo za kifedha za kimtandao kupitia malipo ya fedha kimtandao kupitia mitando yao ya posta.
Afisa mwandamizi wa taasisi ya Bill n Melinda Jamie Zimmerman amesema, “mtandao mkubwa wa posta, hususan maeneo yaliyoko ndani zaidi, ina maana ya kwamba mtandao wa posta uko maeneo ambako wengine hawafiki. Tunaona fursa kubwa zaidi ya mtandao wa posta kuziba pengo na kusaidia kuchochea huduma jumuishi za kifedha. Kupitia FITAF, mashirika ya posta yanaweza kupata msaada wa kiufundi wa unahitajika ili kuona sasa teknolojia za kidijitali zinakuwa asilia.”
Msaada wa kiufundi unaotajwa kwenye mradi huo ni pamoja na mashirika hayo manane ya posta kusaidia kuandaa mikakati ya huduma za fedha kimtandao na kujenga ubia kati ya sekta ya umma na binafsi na kutekeleza suluhu kama vile huduma za benki kimtandao na uwekaji wa akiba kidijitali.
Tayari UPU imetaka wanaotaka kutekeleza awamu ya tatu ya mradi wa FITAF kuwasilisha maombi yao kupitia wavuti huu.