Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mengi yanayojadiliwa Baraza la Usalama yanahusu Afrika hivyo sauti ya Afrika ni muhimu- Kenya

Waziri wa Kenya wa mambo ya nje, Monica Juma wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa
UN News/Assumpta Massoi
Waziri wa Kenya wa mambo ya nje, Monica Juma wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa

Mengi yanayojadiliwa Baraza la Usalama yanahusu Afrika hivyo sauti ya Afrika ni muhimu- Kenya

Amani na Usalama

Kenya ina uzoefu katika masuala ya Usalama na hiyo ni moja ya sababu ambayo imesukuma nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuwania nafasi ya mwanachama asiye wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Hiyo ni kauli ya Waziri wa mambo ya Nje wa Kenya, Monica Juma ambaye wakati akihojiwa na Grace Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya taifa hilo la Afrika Mashariki kuzindua rasmi siku ya Alhamisi kampeni yake ya kuwania nafasi hiyo.

Waziri Juma ametaja miongoni mwa yale watakayoyazingatia ni uwakilishi wa kudumu wa bara Afrika kwenye Baraza la Usalama ambao kwa sasa haupo.

Soundcloud

Halikadhalika Waziri Juma amesema kwamba katika ajenda yao wameweka mambo kumi ambayo watayapa kipaumbele iwapo watapata nafasi hiyo ikiwemo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaundwa na wajumbe 15 ambapo nchi 5 zina ujumbe wa kudumu na kura turufu huku 10 si wajumbe wa kudumu na hazina kura turufu na ujumbe wao huwa ni wa  kipindi cha miaka 2.

Nchi zenye ujumbe wa kudumu ni Marekani,  Uingereza, China, Ufaransa na Urusi.