Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa FAO Tanzania kwa wakulima wa mpunga umebadili maisha ya wakazi

Mpunga ukiwa shambani
IAEA
Mpunga ukiwa shambani

Mradi wa FAO Tanzania kwa wakulima wa mpunga umebadili maisha ya wakazi

Ukuaji wa Kiuchumi

Mradi wa Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO nchini Tanzania wa kutoa mafunzo na kuwezesha vijana na watu wazima kuimarisha kilimo na zao la mpunga umezaa matunda. 

Mradi huo ulianza kwa kuwalenga vijana 150 kwa kutoa mafunzo ya kilimo bora na stadi za maisha ambapo kila kijana alihitajika kuwatafuta vijana wenzake wanne na kuwapa mafunzo na stadi alizopokea ambapo kwa kutumia mbinu hiyo wameweza kufikia vijana 600 kama anavyoelezea Diomedes Kalisa mratibu wa mradi mkoa wa Morogoro nchini Tanzania.

(Sauti ya Dimedes)

Kupitia mradi huo, wakulima wamepokea mashine mpya nne za kukoboa mpunga na kupanga madaraja ya mchele kutokana na ubora wake. Bertha Fredrick Ndikwege ni mnufaika wa mradi

(Sauti ya Bertha)

Uwezeshaji vijana kujiajiri katika kilimo na  kukuza vipato kupitia bora cha mpunga licha ya mafanikio baadhi ya wanufaika umezua hisia tofauti kutoka kwa baadhi ya wenyeji kama anavyosema mkulima kijana Muhesa Kazumba

(Sauti ya Muhesa Kazumba)