Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo jumuishi Ethiopia yaleta matumaini mapya kwa mkimbizi kutoka Yemen

Koat Reath, mkimbizi kutoka Sudan Kusini sasa anaishi Ethiopia ambako pia anafundisha akiamini kuwa elimu ni msingi wa mustakabali wenye nuru kwa taifa lake.
UN News
Koat Reath, mkimbizi kutoka Sudan Kusini sasa anaishi Ethiopia ambako pia anafundisha akiamini kuwa elimu ni msingi wa mustakabali wenye nuru kwa taifa lake.

Mafunzo jumuishi Ethiopia yaleta matumaini mapya kwa mkimbizi kutoka Yemen

Wahamiaji na Wakimbizi

Nchini Ethiopia, mradi wa mafunzo ya ufundi kwa vijana umepatia wakimbizi na wenyeji fursa ya pamoja ya kujifunza, kuchangia katika uchumi wa nchi na pia kuondokana na utegemezi. 

Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, wanafunzi wakiwa darasani. Hawa ni wakimbizi na wenyeji wakijifunza masomo na stadi kadhaa za kazi ikiwemo mapishi, ufundi seremala na ufundi mchundo.

Mradi huu katika chuo hiki cha ufundi cha Nefas Silk unafadhiliwa na shirika la maendeleo la Ujerumani na miongoni mwa wanafunzi ni Hanan Seif Hassan, mkimbizi kutoka Yemen ambaye awali kutokana na umri wake wa miaka 32 alikuwa na hofu kuwa atasomaje utu uzimani.

Hannan anasema kwamba,  “niliona aibu kurejea shule baada ya miaka yote hii lakini nilipoona vile wengine wanajifunza, nikahamasika na kuingia.”

Kadri siku zilivyosonga Hannan alijenga urafiki na Yanchinew Gebeyu, raia wa Ethiopia na shaka na shuku zilitoweka zaidi kama asemavyo Yanchinew ya kwamba,  “watu wanatoka mataifa tofauti na ilikuwa vigumu kuelewana lakini nilifahamu kuwa mambo yatakuwa mazuri baada ya muda.”

Kila asubuhi, Hanan na marafiki zake wanakata vitunguu, wanamenya karoti, wanachemsha kunde, wanapika wali na kuandaa sambusa ambazo huuza.

Akizungumzia wanavyotengeneza, Hannan anasema kwamba, “tunajaza ndani nyama kunde, matunda, tende na hata jibini. Tunaja chochote ndani kama inavyotakiwa, kile ambacho watu wanapenda.”

Mradi huu unasaidia wakimbizi na wenyeji kuibuka na miradi ambapo baada ya miezi 6 ya mafunzo Hannan na Yanchinew waliibuka na mpango wa kibiashara na kuingiza sambusa zao sokoni ambapo kila siku wanaweza kuuza sambusa 200.

Kwa Hannan, Ethiopia imempatia fursa mpya ambazo katu asingaliweza kuzipata nyumbani Yemen na urafiki wake na Yanchiew unakua kila uchao.

Ethiopia inaongoza barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi na mwezi Januari mwaka huu ilipitisha sheria mpya ambayo inawapatia wakimbizi fursa adimu ikiwemo kusajili vizazi, ndoa, vifo na hata kupata ajira na huduma za benki na elimu,