Kuna hatua zilizopigwa Gaza, lakini bado suluhu ni Mataifa mawili-Mladenov

28 Oktoba 2019

Katika siku za hivi karibuni licha ya hali mbaya inayowakabili mamilioni ya wakazi wa Gaza kuha nuru kiasi iliyoonekana hasa katika kupungua upande wa machafuko na uvurumishaji wa makombora japo bado kiuchumi na huduma zingine za msingi vinawatesa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Nickolay Mladenov akitoa taarifa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

“Ingawa machafuko ni sehemu ya maisha ya kila siku Gaza lakini wiki za karibuni tumeshuhudia kupungua kwa machafuko na urushaji wa makombora Gaza. Makubaliano ya utulivu yaliyowezekana kwa juhudi za Umoja wa Mataifa na serikali ya Misri ynaendelea kuzingatiwa . Hata hivyo licha ya hatua hizo kubwa za jumla bado Wapalestina watatu waliuawa na vikosi vya Israel IDF na wengine Zaidi ya 500 kujeruhiwa wakati wa maandamano katika uzio ndani ya Gaza.”

Wajibu kwa pande zote

Mladenov amezikumbusha pande zote katika mzozo kuwa kuendelea kwa machafuko Gaza kuna athari kubwa kwa watoto na jamii nzima na kuvitaka vikosi vya Israel kuwajibika kujizuia na kutumia nguvu tu pale ambapo ni lazima kufanya hivyo.  Na kwa upande wa Hamas amewatolea wito wa kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha usalama kwa watotokwenye Ukanda wa Gaza ikiwemo kuzuia kwa Watoto kutumika na kuwaweka katikahatari kubwa ya machafuko.

Katika muda wote uliojumuishwa katika ripoti hii Mladenov amesema “Maroketi sita yalivurumishwakutokaGaza kwenda Israel na hayakusababisha madhara yoyote na kwa kuongezea kwamara ya kwanza kwa muda wa mwezi mmoja hakuna mashambulizi yoyote yaliyofanywa kwa kutumia Maputo. Wakati huohuo kwenye Ukingo wa Magharibi ikiwemo Jerusalem Mashariki Wapalestina wawili waliuawa akiwemo mtoto mchanga kutokana na gesi ya mabomu ya michozi. Pia amesema Wapalestina 88 wakiwemo Watoto 11 walijeruhiwa katika matukio mbalimbali ikiwemo mapigano, operesheni za kijeshi na ghasia zitokanazo na upanuzi wa makazi ya Walowezi wa Kiyahudi. Pia Waisrael wane wakiwemo wanajeshi wawili wa vikosi vya ulinzi  na Mlowezi mmoja walijeruhiwa.”

Hatari mpya Mashariki ya Kati

Bwana Mladenov amesema hatari mpya ikiibuka katika ukanda wa Mashariki ya Kati mgogoro kati ya Israel na Palestina pia unasalia kuwa moja ya chachu kubwa itikadi kali na kutokuwepo na utulivu.

Ukaliwaji wa rdhi ya Wapalestina unaendelea na hakuna hatua yoyote iliyopigwa katika majadiliano ya suluhu ya Mataifa mawili ambayo badio ni suluhu pekee ya amani ya Mashariki ya Kati. Hili ni janga kubwa la vizazi na vizazi kwa watu wa eneo hilo.

Na mnamo Oktoba 26 kwenye mjadala wa Baraza Kuu Rais Mahmoud Abbas alitangaza nia yake ya kutenga tarehe ya uchaguzi kwa ajili ya Palestina , Mratibu huyo ameongeza kuwa “endapo hilo litafanikiwa basi huu utakuwa uchaguzi wa kwanza kwa Palestina tangu mwaka 2006 ambao utatoa uhalali wa taasisi za kitaifa za Palestina.”

Ameitaka jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mchakato huo endapo utaimarisha Umoja wa kitaifa na sio kuleta mgawanyiko.Hii inajumuisha makubaliano kwa ajili ya uchaguzi kufanyika katika maeneo yote yanayokaliwa ya Palestina kwa kuzingatia sharia ,matakwa bora ya kimataifa ya uchaguzi na makubaliano ya jukwaa la kitaifa ambalo litatokana na maafikiano yaliyopo.

Hali halisi Gaza

Mlademov amesisitiza kuwa hali halisi katika maisha ya mamilioni ya Wapalestina waishio Gaza ni mbaya na inazidi kuzorota na hakuna matumaini ya suluhu ya kudumu. 

Israel imeendelea kupanua ujenzi wa makazi yake kwenye maeneo ya Wapalestina ukiambatana na kupokonya ardhi zao na kubomoa makazi ya Wapalestina kufanikisha hilo hususan Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki.

Hivyo amehitimisha ripota yake kwa kusistiza kwamba “Kama ilivyo kwa Israel na Palestina ,vivyo hivyo kwa eneo zima la Mashariki ya Kati juhudi zetu za pamoja ziongozwe na katiba ya Umoja wa Mataifa Katika kila mgogoro kwenye ukanda huu diplomasia na kuzuia machafuko ni kipengee muhimu sana cha ushirika wetu.Suluhu ya kudumu na endelevu ya amani hata hivyo inaweza tu kutokana na misingi ya haki, jhaki za binadamu na sharia za kimataifa.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud