Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya changamoto zote za watoto wakimbizi tunasaidiana:Anita na Janet 

Mwanafunzi wa kike nchini Uganda akiwasiliana na wanafunzi wenzake
© UNICEF/Zahara Abdul
Mwanafunzi wa kike nchini Uganda akiwasiliana na wanafunzi wenzake

Licha ya changamoto zote za watoto wakimbizi tunasaidiana:Anita na Janet 

Wahamiaji na Wakimbizi

Kutana na Anita na Janet wasichana wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambao wote wana umri wa miaka 13 na wanaishi katika makazi ya wakimbzi ya Kyaka nchini Uganda marafiki na wanasaidiana. Jason Nyakundi na taarifa zaidi

Huyo ni Anita rafiki kipenzi cha Janet akisema wanapopewa kazi za shule za masomo ya saynsi ya jamii humsaidia Janet ambaye pia hulipa fadhila kwa kumsaidia Anita katika somo la Kiingereza. Janet na Aninta wana mengi yanayofanana katika maisha yao, wote wana umri wa miaka 13 na wakimbizi wanaotokea Congo DRC na sasa ni wanaishi ukimbizini nchini Uganda wakiwa maswahiba wakubwa.

Anita anasema kwamba, “mimi najisikia vizuri kwasababu ni rafiki wa Janet, na mi nampenda Anita kwa juu namuuliza maswali ananijibu”

Kwa kushirikiana kwa pamoja mradi wa Elimisha mtoto wa Uganda na shirika la wakimbizi la UNHCR, wanatoa vifaa vya shule, vifaa vya usafi na elimu bora, ili watoto wengine kama Janet na Anita waweze kupata elimu na uzoefu wa kubadili maisha yao.

Anita ingawa ni mtoto bado ana ndoto akisema, “mimi napenda kuwa daktari niwe na hudumia watu, hadithiyangu inaishia hapo. Kwaheri”.