Guterres ataka mshikamano zaidi kudumisha amani na kujenga mustakabali bora kwa wote

24 Oktoba 2019

Amani, usalama, upendo na mshikamano ndio msingi wa mustakabali wa dunia, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya Umoja wa Mataifa hii leo.

Kupitia ujumbe wake wa siku ya Umoja wa Mataifa hii leo Oktoba 24 Guterres amesema siku hii inajikita zaidi katika kuaangazia malengo makuu ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa  uliopitishwa siku kama hii miaka 74 iliyopita na kwamba “licha ya hali ya changamoto kubwa tulizo nazo, mkataba huo unabaki kuwa nanga yetu ya maadili ya pamoja. Wakati huu wa mabadiliko mengi sana, Umoja wa Mataifa umejikita katika kuangazia matatizo halisi ya watu halisi, tunafanya bidii ili kuwa na usawa katika utandawazi na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.”

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unapigania haki za binadamu na usawa wa kijinsia huku ukikana chuki ya aina yoyote.Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa ukihusisha wadau mbalimbai unajitahidi kudumisha amani huku ukitoa msaada wa kuokoa maisha kwa milioni ya watu wanaoathirkia na vita vya silaha.

Amesisitiza kuwa shirika la Umoja wa Mataifa lenyewe linazidi kuwa thabiti na kuwajibika linaponapoendelea kuongeza msaada kwa nchi zinazouhitaji. Mwaka ujao Guterres amesema Umoja wa Matiafa unaadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwake na maadhimisho hayo ya kihistoria ni wakati muhimu wa kujenga mustakabali wa dunia, kwa pamoja na kwa amani.

Ametoa wito kwa kila mtu kujiunga na mjadala huo akisema “kwa pamoja hebu na tuendeleze ustawi wetu sisi kama binadamu.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter