Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushindi huu ni kwa Watoto wote wa kike Tanzania:Gyumi

Rebeca Gyumi kutoka Tanzania, mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana na mshindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu 2018.
UN Tanzania/ Stella Vuzo
Rebeca Gyumi kutoka Tanzania, mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana na mshindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu 2018.

Ushindi huu ni kwa Watoto wote wa kike Tanzania:Gyumi

Haki za binadamu

Mahakama ya rufaa  kuu nchini Tanzania leo imekazia hukumu ya mahakama kuu nchini humo kwamba vifungu vya Sheria ya ndoa ya nchi hiyo vinapingana na Katiba kwa kuweka umri tofauti wa kuoa au kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume. Na hivyo kuitaka serikali kubadili sheria hiyo ambayo ni baguzi kwa watoto wa kike ndani ya mwaka mmoja.

Rebecca Gyumi mkurugenzi mtendani wa msichana initiative na mshindi wa tuzo ya shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF amekuwa msitari wa mbele kupigania mabadiliko hayo kwa kusimamia mkataba wa Umoja wa Mataifa wa haki za mktoto unaosisitiza kuwa mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka 18 ni mtoto hivyo hawezi kuolewa. Akizungumza na Idhaa hii pubnde baada ya kutoka mahakamani amesema huu ni ushindi mkubwa

(SAUTI YA REBECCA -1)

Na je safari ya kufikia hukumu hii ilikuwaje?

(SAUTI YA REBECCA- 2)