Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama limewataka viongozi Sudan Kusini kutorejea kwenye machafuko

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakutana na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir mjini Juba.
UNMISS/Isaac Billy
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakutana na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir mjini Juba.

Baraza la Usalama limewataka viongozi Sudan Kusini kutorejea kwenye machafuko

Amani na Usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekuwa ziarani nchini Sudan Kusini tangu mwishoni mwa wiki ikiwa ni wiki tatu tu kabla ya serikali mpya ya umoja wa kitaifa inayotarajiwa kuundwa nchini humo.

Walipowasili katika mji mkuu Juba jana Jumapili wajumbe hao walilakiwa na wawakilishi wa serikali na viongozi wa juu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kabla ya kufanya mkutano na makundi ya kina mama na asasi za kiraia ili kusikiliza uzowefu wao husu vitta na mchakato wa amani.

Miongoni mwa wajumbe hao wa Baraza la Usalama ni balozi wa kudumu wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa Jerry Mathews Matjila amesema “Baraza la Usalama limeelezea hatua kubwa zilizopigwa kuboresha hali ya usalama sudan kusini hususan kwa raia wa kawaida katika mwaka mmoja uliopita kutokana na makubaliano ya amani na kusitisha mapigano. Pia imetambua kupungua kwa machafuko ya kisiasa hali ambayo imewezesha maelfu ya watu kurejea nyumbani na kuchangia watu 594,000waliokuwa wametawanywa na machakufuko kurejeza makwao, mbali ya hayo imewezesha huduma za kibinadamu kuwafikia walengwa na kuongeza biasha miongoni mwa watu wa kawaida.”

 

Chini ya mkataba wa amani uliotiwa saini Septemba mwaka 2018 , serikali mpya ya mpito ya Umoja wa Mitaifa inatarajiwa kuundwa 12 Novemba  2019. Hata hivyo baadhi ya masuala ambayo hayaajifikiwa yanathibitika kuwa kikwazo katika mchakato huo ikiwemo maamuzi kuhusu taifa lijalo na mipaka na pia uunganishwaji wa vikosi vya usalama.

Kiongozi wa upinzani Riek Machar amesema hatojiunga na serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa hadi pale uunganishwaji wa vikosi hivyo utakapofanyika na kusema “Ndio IGAD katika azimio lake imesema kwamba ifikapo 12 Novemba inapaswa kuwe na serikali mpya iitwayo serikali mpya ya mpito ya Umoja wa kitaifa , lakini mambo yanayohitajika kwa ajili ya uundwaji wa serikali hiyo hayapo. Mfano tukiunda serikali tarehe 12 Novemba unajua nini kitakachotokea? Usitishaji mapigano ambao tumekuwa tukiufurahia karibu mwaka sasa utasambaratika”

 

Wajumbe wa Baraza la Usalama wamekuwa na mazungumzo marefu na Rais wa Sudan kusini Salva Kiir pamoja wa wadau wengine waliotia saini mkataba huo wa amani akiwemo Dkt. Riek Machar ambaye alisafiri kurudi nyumbani kwa sababu ya mkutano huo. Na wajumbe wa Baraza la Usalama walikuwa na ujumbe bayana kwamba pande kinzani zinapaswa kuunda kuunda serikali jumuishi kama zilivyoahidi.

Kelly Craft ni mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa “Baraza la Usalama linatoa wito kwa pande zote kwenye makubaliano ya amani kuharakisha utekelezaji wa mchakato wa mpango wa mpito wa vikosi vya usalama na kuendelea na mjadiliano kuhusu masuala kadhaa na mipaka ya nchi na kuunda kwa amani serikali ya mpito ya Umoja wa Kitaifa ifikapo Novemba 12. Tumesikitishwa na tarifa ya Dkt.Riek Machar kwamba makubaliano ya usitishaji mapigano huenda yakawa hatarini”.

 

Baraza la Usalama limezitaka pande zote kuonyesha uongozi imara ili kuhakikisha kwamba taifa hilo halirejei nyuma kwenye machafuko. Bi. Craft amesisitiza kuwa “Kuna fursa kwa viongozi wa Sudan kusini kufanya muafaka wa kisiasa na kusonga mbele katika hatua inayofuata ya mchakato wa amani katika njia inayoaminika, ya wazi na ya uwajibikaji.

Kuna fursa kwa watu wa SudanKusini kuishi huru bila machafuko ya kisiasa na kuwa na mustakabali bora wa kiuchumi kwa ajili ya watoto wao.

Baraza la Usalama limeahidi kuendelea kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa ili kuhakikisha kwamba amani ya kudumu inapatikana Sudan Kusini.