Serikali na kampuni za intaneti wameshindwa kuzuia kauli za chuki mtandaoni: UN

21 Oktoba 2019

Katika ripoti ya kihistoria iliyotolewa leo ili kusisitiza viwango vya kisheria kukabiliana na kauli za chuki mtandaoni, mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza ametoa wito kwa serikali na kampuni kuondokana na sera zisizo na viwango na mbinu zisizo endelevu kupambana na changamoto hiyo na badala yake kuelekeza sheria zao na utendaji wao dhidi ya kauli za chuki kwa kuzingatia sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Mtaalam huyo wa uhuru wa maoni na kujieleza David Kaye katika ripoti yake inayowasilishwa leo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema “ongezeko la chuki mtandaani linatoa changamoto kubwa kwa kila mtu hususan kwa watu ambao wametengwa wanachukuliwa kuwa ndio chambo kikubwa, na kwa bahati mbaya nchi na makampuni wameshindwa kuzuia kauli za chuki kuwa habari bandia zijazo” hali ambayo amesema ni tata na iliyotumika sana kisiasa likilenga unyanyasaji wa serikali na siri ya makampuni.

Bwana Kaye ameongeza kuwa "Kauli za chuki za mtandaoni sio kwamba hazina madhara kwa sababu ziko mtandaoni,badala yake kauli hizo za chuki mtandaoni, kutokana na kasi na usambazaji wake wa haraka, zinaweza kusababisha madhara makubwa nje ya mtandao na malengo yake karibu kila wakati ni kuwanyamazisha wengine. Swali sio endapo tunaweza kushughulikia unyanyasaji kama huo. Ni jinsi gani ya kufanya hivyo kwa njia inayoheshimu haki za kila mtu anafurahia mtandao. "

Hatua za kuchukua

Katika ripoti yake Bwana Kaye amezitaka nchi kutimiza wajibu wake wa kimataifa kwa kugeukia mikataba ya haki za binadamu na tafsiri zinazoongoza za sharia za haki za binadamu zilizowekwa na kamati ya haki za binadamu lakini vilevile mpango wa hatua 2013 wa Rabat.

Ameelezia pia hofu yake hususan kuhusu serikali zinazotumia kauli za chuki ili kubinya uhalali wa watu kujieleza kwa madai kwamba wanakashifu dini, au wanashoshindwa kuelezea na kutekeleza sharia za kupambana na kauli za chuki kwa mujibu wa sharia na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu, ulazima na kiwango chake na pia uhalali wake.

Serikali na umma wana hofu ya kweli kuhusu kauli za chuki mtandaoni, kwani makampuni yanashindwa kuzingatia sheria mpya ambazo zinatotoa shinikizo kwa makampuni ambayo yanashindwa kufuata viwango vya msingi, kuongeza uwezo wa watu hao binafsi dhidi ya maadili ya umma na kuhatarisha uhuru wa kujieleza na wajibu kwa umma.”

Mtaalam huyo maalumu ameongeza kuwa “kampuni vilevile hazichukulii kwa umakini zaidi utekelezaji wa majukumu yake ya kuheshimu haki za binadamu. Ni kwenye majukwaa yao ambako kauli za chuki zinazambazwa kushika kasi na kuwafikia wengi kwa kutumia nyezo ambazo zinathamini kujulikana na idadi ya watu walioona. Ina athari kubwa kwa haki za binadamu na wanashindwa kuunda sera zenye msingi wake katika sharia za haki za binadamu kwama wanavyotakiwa kufanya hivyo na muongozo wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na haki za binadamu.”

Mwelekeo kwa kampuni

Ripoti ya Kaye inayapa makampuni muongozo wa kukabiliana na kauli za chuki mtandaooni kwa mujibu wa misingi ya sheria za haki za binadamu. Inamaainisha pia ukosefu wa tathimini ya athari kwa haki za binadamu katika ngazi zote  za kuzalisha mtandaano, kutoeleweka vyema kwa sheria za kampuni na ukosefu wa uwazi katika mchakato mzima wa kampuni.

Amesisitiza kwamba “Jumuiya ya haki za binadamu imekuwa na majadiliano ya muda mrefu na mitandao ya kijamii na makampuni mengine kuhusu uchumi wa kimtandao, lakini bado makampuni hayakubali kuahidi sera ambazo zinashindwa kutekeleza hatua kwa mujibu wa hulka za msingi wa sheria za haki za binadamu, kuanzia uhuru wa kujieleleza na faragha na mpaka kupinga ubaguzi, kuchochea ghasia na kuchagiza ushiriki wa umma."

Ametoa wito akisema“Kampuni zinazoshindwa kutambua uwezo wake na athari na kuthamini wadau kuhusu matakwa ya umma yanapaswa kuacha tabia hiyo mara moja. Ripoti hii inapatia kampuni nyenzo ya kubadili mtazamo huo.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter