Tanzania tumeazimia kuzipa kipaumbele takwimu-Dkt Akbina Chuwa

21 Oktoba 2019

Wakati siku ya kimataifa ya takwimu imeadhimishwa tarehe 20 Oktoba mwaka  huu, Tanzania inaungana na nchi nyingine kuhakikisha inazipa kipaumbele takwimu katika kupanga maendeleo ya wananchi kwenye juhudi za kuelekea kufanikisha maendeleo endelevu.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, mapema mwaka huu, Mtakwimu mkuu wa serikali ya Tanzania Dkt Albina Chuwa ameeleza jinsi ambavyo takwimu ni suala la kila siku la maisha ya kila binadamu.

“Katika kaya kwa mfano, wakati unapanga matumizi na mapato ya kaya yako, lazima ugawanye ujue kwamba ninunue kitu fulani nitatumia kiasi gani cha fedha. Ile ni takwimu tayari.  Mapato haya nimeyapata niyagaweyeje, shule,niyafanye huku. Tunasema hizo ni takwimu za mapato na matumizi katika kaya. Kwa hiyo hapo ni kwamba mtu ni lazima kwa kawaida uwe na kitabu chako ambacho unapanga matumizi yako na mapati, halafu mwisho wa mwezi unajipanga vizuri sawasawa na mshahara wako uone kwamba uko katika ile hali unayotaka kuishi. Kwa hiyo ile ni takwimu.”

Dkt Chuwa ameongeza kuwa hivi sasa ulimwengu mzima umeazimia kuzipa takwimu kipaumbele katika mipango ya maendeleo

“Tunataka, tumeazimia kuendeleza tasnia ya takwimu duniani. Huu utashi wa kisiasa ulioanza katika Umoja wa Mataifa unashuka hivyo. Angalia mawaziri wetu wa fedha na mipango ya Afrika waliazimia kwamba takwimu ikae pale ju una ndio muongozo wa agenda ya 2020-2063 ya Afrika. Ukienda Tanzania, mpango wa maendeleo wa miaka mitano, kwa hiyo unakuta agenda ya takwimu iko mbele. Mi ninavyomsikia rais wangu anasoma hotuba yake , anatumia takwimu, nasema, ah! Nakushukuru Mungu. Kwasababu sasa takwimu imeingia, siyo suala la zamani watu wanapanga kwa kutumia uzorfu.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter