Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni bora tuzibe ufa badala ya kujenga ukuta, uhasama wa kibiashara kati ya Marekani na China-Guterress

Makao makuu ya Benki ya Dunia, jijini Washington DC.
World Bank/ Simone D. McCourte
Makao makuu ya Benki ya Dunia, jijini Washington DC.

Ni bora tuzibe ufa badala ya kujenga ukuta, uhasama wa kibiashara kati ya Marekani na China-Guterress

Tabianchi na mazingira

Uhasama unaozunguka biashara kimataifa na teknolojia vinaendelea kupanda na jamii ya kimataifa inahitahi kufanya , “kila linalowezekana” kuzuia dunia kugawanyika katika pande mbili zikiongozwa na Marekani na China.

Huo ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumamosi wakati wa mkutano wa kila mwaka wa Benki ya Dunia na shirika la fedha duniani, IMF uliofanyika jijini, Washington DC Marekani.

Akizungumza na kamati ya IMF, Katibu Mkuu amesema, “wakati wa uhasama na majaribio” akiongeza kwamba, “kuna hofu ya uwezekano wa mgawanyiko mkubwa wa chumi mbili kubwa zaidi kugawanya dunia kwa pande mbili kila moja na sarafu yake, sheria za biashara na fedha, mtandao wake na akili bandia na mikakati ya kisiasa ya kikanda na kijeshi.”

Bwana Guterres amesema, “muda haujapita sana kuweza kuepuka mgawanyiko huo, lakini ni lazima tufanye kila liwezekanlo kuzuia hilo na kuwezesha uchumi wa kimataifa unaoheshimu sheria za kimataifa; dunia yenye mataifa mengi yenye nguvu na taasisi thabiti kimataifa kwa mfano Benki ya Dunia na IMF.”

Katibu Mkuu huyo amegusa maeneo matatu ambapo sera za serikali na uwekezaji katika siku zijazo unaweza kuwa na tija. Kwanza hakikisha mifumo ya ushuru ni “janja, na inazingatia mabadiliko ya tabianchi na inaendana na malengo ya maendeleo endelevu na ajenda ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.”

Pili oanisha mfumo wa kifedha kuendana na malengo ya maendeleo endelevu , kwa kuchochea ufadhili wa muda mrefu kutoka kwa umma na sekta binafsi na kurekebisha masharti ya kifedha ambayo yanaweza kuchagiza miradi ya muda mfupi kwenye soko la kifedha.

Tatu, “ni wakati wa kuvunja minyororo ya madeni makubwa yanayofuatiwa na majanga ya madeni”, ikimaanisha kuweka mfumo bora wa kukopesha na kukopa kwa umakini zaidi.

Na ni lazima tulenga mataifa yaliyohatarini ya athari za mabadiliko ya tabianchi, kama vile mataifa yanayoendelea ya visiwa vidogo. Bwana Guterres amesema anaunga mkono pendekezo la kubadili deni kuwa mkopokwa ajili ya kujengea mnepo kama sehemu ya mradi wa deni kwa ajili ya kujenga mnepo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Akiongeza kwamba, “tunahitaji kutoka kwa wazo hadi vitendo. Pamoja hebu tuimarishe azma ya ufadhili kwa ajili ya maendeleo, mabadiliko ya tabianchi na ufadhili ambao ni jumuishi na unaruhusu soko kukua, biashara kuimarika na watu kuishi maisha ya hadhi.”

Fursa kubwa kwajili ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabinchi

Akizungumza kwenye mkutano wa muungano wa mawaziri wa fedha kwa ajili ya mawaziri kwa ajili ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, bwana Guterres amesema kundi hilo la wanachama 44 lililozinduliwa miezi sita iliyopita ilikuwa ni sehemu muhimu kwa ajili ya kukabiliana na dharura ya mabadiliko ya tabianchi.

Kongamano la hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi mwezi uliopita jijini New York ulikuwa umeonyesha "dunia inaamka kwa janga", na "fursa nzuri" katika siku zijazo kupunguza uchafuzi wa hewa, kuokoa mabilioni ya dola kwenye misiba inayosababishwa na ongezeko la joto ulimwenguni, na kufungua faida za kweli za uchumi unaojali mazingira.

Licha ya "pengo kubwa la hatua na fedha" mawaziri wa fedha wanaweza kugeuza wimbi hilo: "Mnakuja mezani na mchanganyiko wa vifaa, pamoja na sera ya ushuru, matumizi yaliyodhibitiwa na bajeti ya hali ya hewa ... Na unaweza kumaliza ruzuku zinazozalisha tija kwa mafuta ya ziada na kuweka njia kwa yale ambayo ningependa kuona kama mwelekeo mkubwa: kuhamisha ushuru kutoka mapato, hadi kaboni. "

Sweden na Colombia tayari zinatumia ushuru wa kaboni; Uganda inatumia mfumo wa bajeti ya mabadiliko ya tabianchi; na kisiwa cha Dominica kimetumia sera ya fedha kuboresha utayari wa atahri za hali ya hewa, kufuatia kimbunga kilichopiga kisiwa hicho.

"Ushirikiano wenu unachukua mbinu yote ya serikali tunayohitaji kwa ajili ya mabadiliko ya kimfumo. Tunahitaji kuwa na mipango kabla ya mkutano wa COP26, ramani za barabara za kiwango cha chini na sera za fedha kwa jaili ya mabadiliko ya kiuchumi, kiteknolojia na nishati ".