Chuki dhidi ya Uyahudi ni sumu ya demokrasia, elimu yahitajika: Shaheed
Chuki dhidi ya Uyahudi ni sumu ya demokrasia, elimu yahitajika: Shaheed
Chuki dhidi ya Uyahudi ambayo ni sumu ya demokrasia na tishio kubwa kwa jamii zote ni lazima ishughulikiwe na nchi zinapaswa kuwekeza katika zaidi katika kuelimisha kuhusu tishio hilo . Kauli hiyo imetolewa leo na mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa dini au imani Ahmed Shaheed alipowasilisha ripoti yake kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya wayahudi.
Katika mjadala huo kuhusu umuhimu wa elimu katika kushughulikia changamoto hiyo Shaheed amesema chuki hiyo dhidi ya Uyahudi inaongezeka miongoni mwa makundi yote ya siasa za mrengo wa kulia na mrengo wa kushoto “Ninashitushwa na kiwango cha ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi vinavyofanywa na wanaohisi watu weupe ni bora zaidi, ikiwemo wanaofuata siasa za kinazi na makundi ya itikadi Kali ya kiislam hasa katika lugha, misemo, picha, unyanyapaa na dhana za kuchochea na kuhalalisha ukatili, ubaguzi na machafuko dhidi ya Wayahudi”. Pia ninatiwa hofu na ongezezo ya maneno ya kupinga ushirika na Wayahudi kutoka katika vyanzo vya mrengo wa kushoto wa kisiasa navitendo vya kibaguzi dhidi ya Wayahudi .
kupinga Uyahudi ni chachu ya kuzidisha chuki ya kimataifa -Ahmed Shaheed mtaalam wa UN kuhusu uhuru wa dini au imani.
Mtaalam huyo ametanabaisha katika ripoti yake kwamba mauaji ya Holocaust wakati wa vita vya pili vya dunia kama ni mfano mbaya halisi wa jinsi gani chuki za kidini na ubaguzi wa rango vinavyoeweza kusababisha mauaji ya kimbari na uharibifu mkubwa wa jamii.
Licha ya mfano huo Sheheed amesenma ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya Uyahudi vimekuwa vikiripotiwa kimataifa ikiwemo machafuko, ubaguzi, hisia za ukatili , na tatizo linaongezewa na kuzagaa kwa hotuba za chuki katika mitandao ya intaneti
Kuwekeza katika elimu
Katika mahojiano maalum na UN News Bwana. Shaheed ameelezea chuki dhidi ya Uyahudi kama ni chachu ya kuzidisha chuki ya kimataifa hali ambayo inatoa changamoto kubwa katika kutokomeza mifumo yote ya kutovumiliana, chuki na ubaguzi kwa misingi ya dini au imani na kuweka hatari kubwa kwa makundi ya walio wachache kila mahali duniani wakiwemo Wayahudi.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo Shaheed amezitaka nchi kuwekeza katika elimu na mafunzo ili kuwezesha uelewa kuhusu chuki dhidi ya Wayahudi.”Elimu ni ufunguo katika kushughulikia masuala haya na kuzuia matukio ya chuki katika siku za usoni.”
Pia amesisitiza kushirikisha vijana ili kuhakikisha kwamba wanaikana chuki dhidi ya Wayahudi na kwamba “muungano wa kimataifa unahitajika kuzungumza bayaka kuhusu chuki dhidi ya Uyahudi na elimu ni nyenzo muhimu kufikia lengo hili.”