Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yapata mafanikio makubwa kwenye chajo mpya dhidi ya ugonjwa wa Ebola

Utoaji chanjo ya Ebola
WHO/S. Hawkey
Utoaji chanjo ya Ebola

WHO yapata mafanikio makubwa kwenye chajo mpya dhidi ya ugonjwa wa Ebola

Afya

Shirika la afya duniani (WHO) linakaribisha  tangazo kutoka kwa shirika la dawa la Ulaya (EMA) kuhusu kuanza kuuzwa kwa chanjo ya rVSV-ZEBOV-GP ambayo imeonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kuwakinga watu kutokana na virusi vya Ebola.

Tangazo la leo  la EMA, ambalo ni shirika la Ulaya lenye wajibu wa kuchunguza madawa yanayotengenezwa na kampuni tofauti, ni hatua kubwa kabla ya tume ya ulaya kutoa leseni kwa matumizi yake

Kuruhusiwa kwa chanjo ya kwanza ya ugonjwa  wa Ebola ni mafanikio kwa afya ya umma na ushuhuda wa ushirikiano  uliopo kati ya wataalamu kote duninia, amesema Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO.

Katika kipindi cha miaka mitano ijayo WHO  imewatuma wataalamu kuchunguza chanjo kutoka kwa watengenezaji kadhaa wa chanjo hizo.

Maafisa wa WHO wakiandaa chanjo ya Ebola huko Butembo DRC.
WHO/Lindsay Mackenzie
Maafisa wa WHO wakiandaa chanjo ya Ebola huko Butembo DRC.

Majaribio ya chanjo hiyo yalianzia wakati wa mlipuko wa Ebola uliotokea magharibi mwa Afrika mwaka 2015. Wakati huo hakukuwa na shirika lolote lililoruhusiwa kuendesha majaribio nchini Guinea wakati wa dharura, serikali ya Guinea na WHO walichukua hatua kuongoza majaribio.

WHO inasherehekea kujitolea  kwa kiwango kikubwa kutoka kwa wengi katika kipindi cha miaka mitano na jitihada za kimataifa zilizochangia mafanikio kama haya katika sekta ya afya ya umma.

Kazi ngumu zaidi ikifanywa na timu ya kimataifa la watafiti, wafanyakazi wa afya, washirika, serikali na wafanyakazi wa nje kama wasafirishaji , watoa chanjo na jamii.

Kwa pamoja walivuka vizuizi. WHO pia inaitambua serikali ya Canada  kwa mchango wake katika jitiha za mapema za kupatikana kwa chanjo hiyo.

Kwenye mkurupuko wa hivi punde nchini Jamhuri ya Demoksrasi ya Congo, zaidi ya watu 236,000 wamechanjwa wa kutumia chanjo ya rVSV ZEBOV GP, iliyotolewa  na Merck kwa WHO wakiwemo zaidi ya wafayakazi  60,000 nchini DRC na Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Burundi.