Viongozi wakuu 30 kutoka sekta za biashara kujiunga na UN kufanikisha maendeleo endelevu

16 Oktoba 2019

Umoja wa Mataifa umetangaza leo kuwa viongozi 30 wenye ushawishi kutoka sekta za biashara watashirikiana katika kipindi cha miaka miwili ijayo katika jaribio la kufungulia matrilioni ya dola kutoka sekta ya kibinafsi kufadhili maendeleo endelevu.

Ushirikiano huo ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa MataifaAntonio Guterres na wawezekaji wa kimataifa katika maendeleo endelevu, uko chini ya usimamzi wa Oliver Bäte, Mkurugenzi Nkuu wa  Allianz, na Leila Fourie, Mkurugenzi Mkuu wa soko la hisa la Afrika Kusini, na unajumusiha pia wakuu wa Bank of America, Citigroup, ICBC, Infosys, Investec, Santander, UBS na mashirika mengine maarufu.

Akizungumzia ubia huu Katibu Mkuu Guterres amesema, "tunakabiliwa na ukosefu wa usawaa unaozidi kuongezeka, uharibifu kutokana na mizozo na majanga na kuongezeka kwa haraka kwa joto duniani. Viongozi hawa wanataka tuchukue hatua za dharura wakisema kuwa kasi yetu iwe ni ya kukimbia na wala si ya kutambaa".

Mkutano mkuu wa mazungumzo kuhusu ufadhili wa maendeleo uliandaliwa kwenye mkutano wa hivi majuzi wa Umoja wa Mataifa, ulioweka wazi dharura kuongeza matumizi wa serikali katika sekta muhimu kama afya, elimu, miundo msingi na mabadiliko ya tabia nchi.

Nchi nyingi zilizostawi hazijatimiza ahadi zao huku masuala kama umaskini, ufisadi, ukwepaji kodi vikichangia ukosefu wa kipato kwenye nchi zinazoendelea.

Fedha za maendeleo hukadiriwa kuwa matrilioni ya dola kwa mwaka na hata kuna ufadhili kutoka sekta zote za umma, bado kutakuwa na kasoro kubwa hali ambayo hufanya ufadhili kutoka sekta za umma kuwa na umuhimu.

Utafiti wa Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa hakuna upungufu wa pesa kutoka sekta ya binafsi ambazo zinaweza kuwekezwa katika maendeleo endelevu. Hata hivyo masuala kadhaa yakiwemo sera na hali yaliko mashirika huathiri kujitolea kwa muda mrefu kunakohitajika.

Kwa mujibu wa Guterres katika kipindi cha miaka miwili ijayo kundi hili, "litaleta suluhu na kufungua milango ya ufadhilia wa muda mrefu na uwekezaji katika maendeleo endelevu , litachangia fedha zaidi kwa nchi na sekta zilizo na mahitaji zaidi, litatafuta njia za kuongeza matokeo bora kutokana na sekta za biashara na pia kuunganisha masuala ya kibiashara na ajenda za maendeleo endelevu za mwaka 2030."

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter