Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa Umoja wa Mataifa Haiti  MINUJUSTH wafunga mlango baada ya miaka 15 ya huduma

Jean-Pierre Lacroix, mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa akitoa taarifa kwenye kikao cha Baraza la Usalama kuhusu Haiti 15 Oktoba 2019
UN Photo/Eskinder Debebe)
Jean-Pierre Lacroix, mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa akitoa taarifa kwenye kikao cha Baraza la Usalama kuhusu Haiti 15 Oktoba 2019

Mpango wa Umoja wa Mataifa Haiti  MINUJUSTH wafunga mlango baada ya miaka 15 ya huduma

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Haiti ulioanza miaka 15 iliyopita kama operesheni za kulinda amani MINUSTAH na kisha MINUJUSTH leo umefunga rasmi pazia baada ya kutoa huduma mbalimbali kwa mamilioni ya watu wa taifa hilo, operesheni ambazo zitaendelezwa sasa na mpango wa kisiasa.

Akizungumza kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu ya siku 90 za mwisho za operesheni ya msaada wa masuala ya haki nchini Haiti MINUJUSTH, Jean Pierre Lacroix  mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa amelitaka wajumbe wa Baraza hilo kutafakari uwepo wa muda mrefu wa Umoja wa Mataifa Haiti na hali inayoendelea hivi sasa nchini humo.

Na ameongeza kuwa kufunga mpango kwa operesheni za ulinzi wa mani Haiti ni kuanza kwa ushirika mpya baina ya taifa hilo na Umoja wa Mataifa kwani “nchi hiyo inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa ukiambatana na changamoto zingine za kijamii na kiuchumi, ambazo pia zinaathiri mazingira ya usalama. Kuna mzunguko wa changamoto zilizoshuhudiwa na taifa hilo mara nyingi”

Kinachoendelea Haiti

Akifafanua kuhusu kinachoendelea hivi sasa nchini Haiti Lacroix amesema serikali ya nne ya Rais Jovenel Moïse bado haijathibitishwa na bunge na machafuko na ghasia za kisiasa zimekuwa zikishuhudiwa. Uchaguzi wa bunge hauwezi kufanyika katika hali ya sasa ya mvutano wa kisiasa na tayari jukwaa limeandaliwa la pengo la uongozi mwanzoni mwa mwaka 2020.

Na wito wa Rais wa kufanya majadiliano ya kitaifa na kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa yanachukuliwa na wapinzani kama yamechelewa.

Lacroix amesisitiza kwamba “kutoaminiana kunafanya kuwa vigumu kufikia makubaliano nab ado inasuburiwa kuona kama uteuzo wa waziri mkuu Evans Paul uliofanyika Oktoba 9 kwa ajili ya kusaka utangamano na wapinzani utaweza mazingira ya kutatua matatizo na kuafikiana.”

Hali ya usalama

Akigeukia hali ya usalama nchini Haiti mkuu huyo wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa amesema  hali imezidi kudorora katika miezi ya hivi karibuni na idadi kubwa ya raia wan chi hiyo hawaridhishwi na viongozi wao na pia hali ya kiuchumi na kijamii nchini humo.

Ameongesa kuwa watu hao wamekuwa wakikusanyana kwa ajili ya maandamano  na kudai mabadiliko na wengine wako tayari kutumia ghasia ili kufikia malengo yao ya kisiasa. Hadi sasa amesema takriban watu 30 wamearifiwa kuuawa wakati wa maandamano kati ya tarehe 15 Septemba na 9 Oktoba, lakini pia matukio ya hotuba za chuki na matumizi ya vyombo vya Habari kuchochea ghasia yameongezeka.

Mbali ya hayo amesema jeshi la polisi la Haiti linakabiliwa na mtihani mkubwa wa kudhibiti usalama bila kuwa na msaada wa kimataifa. Limefanya vizuri lakini kuendelea kuwepo na msaada wa ushauri kutoka Umoja wa Mataifa na msaada wa vifaa kutoka kwa wadau wengine bado kunahitajika.

Changamoto za ziada

Wakati huohuo Lacroix amesema watu wa Haiti ambao bado wanahaha na sintofahamu , hivi sasa wanakabiliwa na changamoto zingine Zaidi na kutokuwa na usalama ambavyo vinaingilia operesheni za kibinadamu. Hospitali, vituo vya Watoto yatima, vituo vya ulinzi wa raia na huduma zingine za dharura zimeathirika vibaya na hali ya usalama na nyingi zinatoa huduma nusunusu kutokana na upungufu wa mafuta , kukosekana kwa maji safi na madawa. Akitoa wito kwa pande zote kinzani nchini Haiti kulaani machafuko na kuyaacha , Lacroix amekaribisha uteulzi uliofanywa na Katibu Mkuu wa mwakilishi mpya wa Umoja wa Mataifa Haiti bi. Helen La Limewa Marekani na kuwataka wadau wote wa Haiti kufanyakazi kwa ushirikiano na kulinda hatua nzuri ambazo zimepigwa katika nchi hiyo.

Je ni muafaka UN kuondoka Haiti hivi sasa ?

Bwana. Lacroix amesema hali ya sasa si muafaka kumalizia mayo baada ya miaka 15 ya operesheni za ulinzi wa amani  nchini humo, hata hivyo ni muhimu kufikiria mchango mkubwa uliofanywa nan a operesheni za ulinzi wa amani nchini humo katika nyanja mbalimbali hususani katika utawala wa sheria. Msaada kwa jeshi la polisi la Haiti umesaidia kuleta mabadiliko makubwa nchini humo huku idadi ya mauaji ikipungua kwa karibu nusu kati yam waka 2004 na 2019. Pia kumekuwa na mabadiliko makubwa katika upande wa masuala ya haki na mabadiliko ya muundo wa utawala yakifungua njia usajili wa askari wa mahakama wakiwemo wanawake kwa msaada wa Umoja wa Mataifa. Kupitia mipango yote miwli MINUSTAH na MINUJUSTH. Mipango hii miwli pia imesaidia kuimarisha haki za binadamu na kuhakikisha uwajibikaji kwa waathirika wa ukiukaji wa haki za binadamu .

Masuala ya urithi

Lacroix amesema kuondoka kwa MINUJUSTH kumefungua mlango wa ofisi mpya ya Umoja wa Mataifa Haiti BINUH ambayo itaendelea kufanyakazi na serikali na wadau wengine kuhusu masuala ya urithi kutoka kipindi cha ulinzi wa amani kama vile kutokomeza kipindupindu na kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kingono na ukatili mwingine ikiwemo kesi za kutambua baba wa mtoto ni nani.

Naye afisa wa ubalozi wa Haiti kwenye Umoja wa Mataifa Patrick Saint-Hilaire amezungumzia haja ya kuendelea kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama ambavyo pia vinahitaji vifaa muafaka na vitu vingine. “Ni muhimu sana kw amalaka ya serikali kurejeshwa haraka kwa mpango ambao sio wa umwagaji dam una usio na kikomo katika maeneo yote ambayo kwa bahati mbaya yanaelezwa kutokuwa na utawala wa sheria.”

BINUH inaashiria mpito wa kutoka kwenye ulinzi wa amani kuelekea ujenzi wa amani na ofisi hiyo ityakuwa na kipimo ambacho kinamulika malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Bwana Lacroix amesema “Hatua zilizopigwa haiti katika miaka 15 iliyopita ni kubwa lakini mafanikio ya kuwa na utulivu bado hayajatimia na ni lazima mizizi yake itokane na demokrasia na maendeleo. Kuanza kwa operesheni za BINUH kesho ni kurejea ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha utulivu na mafanikio kwa Haiti.”