Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 800 kote duniani wanakabiliwa na njaa na kutomudu mahitaji ya lazima ya chakula:WFP

Picha ya UN
OCHA/Franck Kuwonu
Picha ya UN

Watu milioni 800 kote duniani wanakabiliwa na njaa na kutomudu mahitaji ya lazima ya chakula:WFP

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema zaidi ya watu milioni 800, ikiwa ni sawa na mtu 1 kati ya 9 kote duniani wanakabiliwa na njaa na kushindwa kumudu mahitaji ya msingi ya chakula. 

Taarifa hiyo ya WFP iliyotolewa kabla ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani hapo kesho Oktoba 16 inasema asilimia kubwa ya sababu zinazosababisha njaa zinasalia kuwa zilezile ambazo ni vita, mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi na pengo la kiuchumi au kutengwa kiuchumi.

Hivi sasa shirika hilo linasema linafanya kila liwezalo kufikisha msaada wa chakula kwa zaidi ya watu milioni 80 walioathirika zaidi na njaa katika nchi zaidi ya 80 duniani , zikiwemo Yemen, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Mkuu wa masuala ya kiuchumi na naibu mkurugenzi wa FAO Arif Hussain anasema na nuru bado iko mbali katika suala hilikwa bahati mbaya ni kwamba bado kuna mwaka mwingine mmoja wa hadithi ileile, hivyo watu ambao wametengwa, ambao walikuwa masikini mwaka jana, ni masikini zaidi mwaka huu. Na wako kabisa katika maeneo mengi, hususani katika maeneo yenye vita na wanategemea msaada wa chakula. "

Kwa mujibu wa WFP idadi ya watu wenye lishe dunia mwaka jana iliongezeka na kufikia milioni 821 ikiwa ni zaidi ya idadi ya watu wote wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Japan kwa pamoja. Na kwamba takriban watu bilioni 2 wanaishi kwenye nchi ambazo maendeleo yanakabiliwa na changamoto ya vita, kutokuwepo utulivu na kiwango cha juu cha machafuko na asilimia 60 ya watu wote wanaokabiliwa na njaa wako katika nchi zenye vita.