Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mameya wa miji ndio wahudumu wa kwanza wa mabadiliko ya tabianchi-Guterres

Lima, mji mkuu wa Peru, Amerika Kusini.
World Bank/Franz Mahr
Lima, mji mkuu wa Peru, Amerika Kusini.

Mameya wa miji ndio wahudumu wa kwanza wa mabadiliko ya tabianchi-Guterres

Ukuaji wa Kiuchumi

Mameya wa miji ndio wahudumu wa kwanza linapotokea dharura ya mabadiliko ya tabianchi amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ijumaa kwenye mkutano wa kimataifa wa mameya unaofanyika mjini Copenhagen.

Katika hotuba yake kwenye jukwaa la C40 la mameya wa miji  wanachama hatua bunifu za sasa za kupunguza ongezeko la joto duniani, Katibu Mkuu amesema kwamba “miji ambayo ina jumla ya karibu nusu ya watu wote duniani , ambayo ina eneo kubwa la uchafuzi wa hali ya hewa iko msitari wa mbele kuelekea maendeleo endelevu na jumuishi.”  Ameongeza kuwa raia wa mijini wanawaangalia mameya wao katika kuifanya miji kuwa mahali bora pa kuishi, yenye mshikamano na inayozalisha ajira.

Akiwakumbusha washiriki wa jukwaa hilo tishio kubwa linalosababishwa na dharura ya mbadiliko ya tabia nchi na haja ya kuchukua hatua haraka ili kukabiliana na mabadoliko ya tabianchi katika ngazi zote bwana Guterres amesema katika mkutano wa hatua dhidi ya mbadiliko ya tabianchi mwezi Septemba, nchi 70 na miji takribani 100 walitangaza mikakati ya kuimarisha mipango yao ya kitaifa ya kupunguza utoaji wa hewa chafuzi ifikapo 2020.

Hata hivyo amesema “baadhi ya nchi ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa gesi chafuzi ya viwandani bado hawajajitoa kwa dhati kuhakikisha wanaondoa hewa chafuzi ifikapo mwaka 2050”. Na kwa kuwa kuna biashara, miji na jamii zinayokuwa kwa kasi kuliko serikali Katibu Mkuu ametoa wito kwa viongozi wa mijini kuendelea kutoa shinikizo kwa mamlaka za serikali kuongeza malengo ya kukabiliana na tabianchi.

Amesisitiza kuwa miji ni kitovu cham bio za kupunguza utoaji wa hewa chafuzi na athari za kukua kwa kasi bila kuwa na mipango Madhubuti ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zitakuwa kubwa.

Guterres amekaribisha juhudi za sasa zinazofanywa na miji hiyo 40 C40 kama vile kuchagiza afya bora, milo ambayo inajali mazingira na kukabiliana na uchafuzi wa hewa.

Utafiti wa hivi karibuni uliendeshwa na C40 umeonyesha kwamba kula milo endelevu na kuepuka utupaji wa chakula kunaweza kupunguza hewa chafuzi itokanayo na chakula kwa zaidi ya asilimia 60.