Tatizo la kutokuwa na utaifa lapata msukumo mpya:UNHCR

11 Oktoba 2019

Katika hatua ya kihistoria vita vya kimataifa dhidi ya hali ya kutokuwa na utaifa vyapata msukumo mpya baada ya nchi, asasi za kiraia na mashirika ya kitaifa na kimataifa zaidi ya 85 kutoa mamia ya ahadi mpya kutokomeza tatizo hilo ambalo ni sababu kubwa ya mamilioni ya watu duniani kunyiwa hali zao za binadamu.

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wamepokea zaidi ya ahadi 300 kwenye mkutano kuhusu kutokuwa na utaifa unaofanyika Geneva Uswis ujulikanao kama “Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu kutokuwa na utaifa” ukiwa ni sehemu ya mikutano ya kamati ya utawala wa UNHCR inayofanyika kila mwaka.

Shirika hilo linasema idadi hiyo ya ahadi sio kitu cha kawaida kufanyika katika mkutano mmoja.Miongoni mwa ahadi hizo zilizotolewa 220 zimetoka kwa nchi zaidi ya 55 zilizokubali kubali au kuridhia mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu kutokuwa na utaifa ili kuwezesha watu wasio na utaifa kufanywa wazawa, kuzuia kutokuwa na utaifa kwa kukomesha ubaguzi wa kijinsia kwa kuweka sheria za kitaifa, kuhakikisha usajili wa watoto wanapozaliwa kimataifa , kutoa ulinzi kwa watu wasio na utaifa  na kuanzisha ukusanyaji wa takwimu katika jamii ya wasio na utaifa. Akizungumzia umuhimu wa hatua za wiki hii Kamishina mkuu wa UNHCR Filippo Grandi amesema  “Tunafikia wakati nyeti sana katika juhudi za kimataifa ili kukomesha kutokuwa na utaifa. Wiki hii imedhihirisha kwamba kuna kiwango kisischo cha kawaida cha utashi wa kisiasa na ahadi za kutatua tatizo hili na kulizuia kutoibuka ."

Anmeongeza kuwa “ni muhimu sana ahadi hizo sasa kuwa hatua , tutaongeza juhudi zetu kuzisaidia nchi kutimiza malengo ya kutokomeza tatizo la kutokuwa na utaifa.”

UNHCR imeitisha mkutano huo wa ngazi ya juu kuzungumzia hali ya kutokuwa na utaifa ikiwa ni katikati ya muda wa kampeni yake ya miaka 10 ya kimataifa ya #IBelong ambayo ilizinduliwa mwaka 2014 kwa lengo la kukomesha kabia tatizo hilo la kutokuwa na utaifa ifikapo mwaka 2024.

Jumatatu wiki hii Angola na Colombia zimekuwa nchi za hivi karibuni kujiunga rasmi na mkataba wa kutokomesha hali ya kutokuwa na utaifa.  Duniani kote kuna takriban watu milioni 3.9 wanaojulikana rasmi kutokuwa na utaifa lakini kwa mujibu wa UNHCR idadi halisi ni kubwa zaidi ya hiyo.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter