Mradi wa nyumba salama wa UNICEF ni mkombozi kwa wasichana wanaokimbia ukeketaji Kenya

Mwanamke akiwa ameshikilia kisu kilichotumika kwenye ukeketaji.
UNICEF/Catherine Ntabadde
Mwanamke akiwa ameshikilia kisu kilichotumika kwenye ukeketaji.

Mradi wa nyumba salama wa UNICEF ni mkombozi kwa wasichana wanaokimbia ukeketaji Kenya

Haki za binadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wameanzisha nyumba salama kwenye jamii ya wakuria nchini Kenya  kama sehemu ya kukabiliana na tatizo la ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake, FGM.

Katika jamii ya wakuria ukeketaji ni moja ya mila ya kuashiria kuingia utu uzima ambayo analazimika kupitia msichana kwa ajili ya kukubalika kwenye jamii na hatimaye kuolewa huku asilimia 78 ya wasichana wakilazimika kukeketwa.

Kwa kawaida wakati wa msimu wa ukeketaji wasichana hutoroka na kukimbilia vituo vya kuwahifadhi ambavyo ni taasisi ndani ya jamii. 

Hata hivyo kuwaunganisha wasichana hao na familia zao ni changamoto baada ya msimu huo na ndipo UNICEF imeingilia kati na kuziba pengo hilo na kuweka mbadala wa nyumba salama. 

Esther Soguta ni mama ambaye anawahifadhi wasichana waliokimbia kitendo cha ukeketaji huku yeye binafsi akiamua kuwaepusha wanae na tendo hilo.

(Sauti ya Esther)

Elizabeth Soguta ni binti yake Esther ambaye ana umri wa miaka 14 huku bado akiendelea na masomo yake.

(Sauti ya Elizabeth)

Uunngwaji mkono na wanaume katika jamii ni muhimu na kuna baadhi ya wanaume ambao wamejitokeza, mumewe Esther, John Soguta ni baba anayesimamia nyumba hizo salama kwa kushirikiana na mkewe.

(Sauti ya John)

Mradi wa kuweka nyumba salama ndani ya jamii ni muhimu kwani pia linashirikisha wanajamii na pia kutuma ujumbe kwa mangariba kwamba jamii inapinga vitendo hivyo na kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wasichana ambao hawajakeketwa.