Matajiri Afrika wawekeze kwa vijana Afrika-UNCTAD

3 Oktoba 2019

Lengo la kuanzisha ubia kati ya Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD na mjasiriamali Jack Ma kutoka Uchina ni kukusanya vijana kutoka nchi zinazoendelea na kuwawezesha kupaza sauti kuhusu mambo ambayo wangetaka yafanyike ili kurahisisha utendaji wa biashara mtandaoni.

Kauli hiyo ni ya Katibu Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi katika mahojiano maalum nami hivi karibuni kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. 

Dkt. Kituyi alinieleza kuwa utaratibu ambao wanafanya kufuatia ubia huo ikiwemo kutoa ruzuku kwa baadhi ya vijana

(Sauti ya Dkt. Kituyi)

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo amekwenda mbali zaidi na kutoa changamoto kwa matarjiri kuwekeza katika kuimarisha ujuzi wa vijana akisema

(Sauti ya Dkt. Kituyi)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud