Mkuu wa WHO azuru visiwa vya Bahama na kutoa wito wa msaada zaidi wa kibinadamu

2 Oktoba 2019

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO amezuru maeneo yaliyoathirika vibaya na kimbunga katika visiwa vya Bahama na kutoa wito wa msaada zaidi wa kibinadamu kwa waathirika wa kimbunga hicho.

Mkurugenzi huyo Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema “Tunahitaji kuwekeza zaidi katika mifumo ya mnepo wa kukaboiliana na mabadiliko ya tabianchi baada ya kuangalia kwa karibu uharibifu uliosababishwa na kimbunga Dorian , mamia ya watu wametoweka baada ya janga hilo la asili kupiga visiwa vya Bahama Septemba Mosi”

Mkurugenzi huo mkuu wa WHO ametoa wito kwa dunia kuungana kwa ajili ya visiwa vya Bahama katika zahma hii ya athari za kimbunga Dorian.” Janga hilo liliikumba nchi hiyo Septemba Mosi, na kuathiri watu 75,000. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa karibu waathirika 1,500 nado wanaishi katika malazi ya muda na wengine 600 hbado hawajulikani waliko. Hadi kufikia leo vifo 56 vimethibitishwa.”

Huduma

Katika mwisho wa ziara yake katika visiwa hivyo vya Abaco na Grand Bahama, Dkt. Tedross amesema janga hilo la kimbunga “sio tuu limegharimu maisha ya watu wengi na kuishi kwao , bali pia imesababisha uharibifu mkubwa katika miundombinu bali pia kuzinyima jamii huduma za msingi katika wakati muhimu sana.”

Hadi leo Jumatano mkuu wa WHO amekuwa katika maeneo yaliyoathirika zaidi na kimbunga Dorian ambako anatathimini athari za kiafaya. Kwa Dkt. Tedros zahma hii ni “kumbusho lingine kwamba  la haraka kwamba sababu za mabadiliko ya tabianchi zinapaswa kushughulikiwa haraka. Inasikitisha kushuhudia jamii zilivyoathirika pamoja na familia zao, zimepoteza kila kitu , marafiki, wapendwa wao, nyumba zao, na fursa ya kupata huduma muhimu.”

Picha ya UN/Elma Okic
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva

 

Akiwa katika visiwa hivyo vya Bahama Dkt. Tedros amekutana pia na maafisa wa serikali akiwemo gavana mkuu. Amepongeza maandalizi yaliyofanyika, hatua zilizochukuliwa na juhudi zilizofanyika kupunguza athari.

Maeneo aliyotembelea mkurugenzi Mkuu wa WHO ni pamoja na Abaco na visiwa vikuu vya Bahama, akiambatana na wariri wa afya w anchi hiyo Duane Sands ambako alishuhudia uharibifu mkubwa na athari zinlizosababishwa na kimbunga Dorian kwa familia na miundombinu ikiwa ni pamoja na vituo vya afya ambavyo vimesambaratishwa kabisa , ikiwemo vifaa tiba, madawa na miundombinu kama nishati ya umeme na maji. Shirika la afya kwa nchi za Amerika PAHO limepeleka wafanyakazi 20 na timu tano za huduma ya dharira ya kitabibu kwenda kusaidia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud