Gillian Triggs ashika hatamu rasmi kama msaidizi mwandamizi wa ulinzi UNHCR

30 Septemba 2019

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limemtangaza Gillian Trigss kutoka nchini Australia kuchukua hatamu rasmi kama Kamishina msaidizi mwandamizi mpya wa wakimbizi kwa ajili ya masuala ya ulinzi.

Bi. Triggs ambaye kuanzia sasa maskani yake ya kazi yatakuwa kwenye makao makuu ya UNHCR Geneva, Uswis hadi siku za hivi karibuni alikuwa na nyadhifa mbalimbali ikiwemo makamu mkuu wa chuo, profesa katika chou kikuu cha Melbourne na Rais wa tume ya haki za binadamu ya Australia, na amepokea kijiti hicho kutoka kwa Volker Türk ambaye aliondoka UNHCR mwezi Julai mwaka huu kwenda kuanza jukumu jipya msaidizi wa Katibu Mkuu kwa ajili ya kuratibu mikakati kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York.

Katika wadhifa wake mpya Bi. Triggs atasimamia kazi za UNHCR za ulinzi kwa mamilioni ya wakimbizi, wakimbizi wa ndani, watu wasio na utaifa na watu wengine ambao hali zao zinatia mashaka.

Naibu Kamishna Mkuu, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa operesheni, na Kamishna msaidizi mwandamizi wa ulinzi kwa pamoja wanajumuisha nafasi tatu za juu zinazomuunga mkono Kamishna mkuu katika kutekeleza majukumu yake.Akizungumza kuanza kwazi rasmi kwa Gillian, kamishna mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi amesema “Nina furaha kwamba Gillian amejiunga nasi na katika wakati muhimu sana tukijiandaa kwa komamano la kimataifa la wakimbizi mwezi Disemba. Kukiwa na idadi kuwa ya watu walazimika kukimbia makwao leo hii haja ya kupata suluhu na mfumo wa ulinzi wa kimataifa imekuwa ni changamoto kubwa na kwa Maisha ya watu wengi. Tunamkaribisha kwa moyo mkunjufu UNHCR.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud