Asilani hatutotiwa woga na vitisho:China

Wang Yi, waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya watu wa China akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 74
UN Photo/Loey Felipe
Wang Yi, waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya watu wa China akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 74

Asilani hatutotiwa woga na vitisho:China

Masuala ya UM

Katika hotuba yake kwenye mjadala Mkuu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa Diwani wa jimbo na waziri wa mambo ya nje wa Uchina ametangaza kwamba nchi yake asilani haitotiwa woga na vitisho au kukubali shinikizo wakati inapokabiliwa na changamoto za ulinzi.

Wang Yi ameuambia mjadala huo wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kwamba China imedhamiria kutatuza mivutano ya biashara na tofauti zilizopo ”Kwa utulivu, fikra makini na kwa ushirikiano ,lakini pia kwa uvumilivu mkubwa na nia njema.”

Hata siku ya Jumanne kwenye mjadala Mkuu Rais wa Marekani Dornald Trump aliliambia Baraza Kuu kwamba hatokubali "mkataba wa mbaya wa biashara " na China wala kutarajia mkataba mzuri.

Katika majibu yake, Bwana Wang amesisitiza kwamba "iwapo upande mwingine utatenda kwa nia mbaya tutalazimika kuchukua hatua muhimu kulinda haki na maslahi yetu halali, na kutetea haki za kimataifa."

Akiangazia utimizaji wa miaka miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa Uchina mnamo 2019, Bwana Wang amesisitiza kwamba "Wachina milioni 850 wamtokomeza umaskini, na mamia ya mamilioni yaw engine wamejiunga na kikundi cha kipato cha kati."

Kuhusu mafanikio ya kidiplomasia ya China, Waziri huyo wa Mambo ya nje amesema kwamba Uchina imeinua amani ya ulimwengu na ustawi kupitia maendeleo yake.

Amesisitiza kwamba "China itaendelea kuzingatia kanuni za misingi ya usawa na kutokuingilia uhuru wa mambo ya ndani ya nchi nyingine kama ilivyoainishwa kwenye katika ya Umoja wa Mataifa “

Wakati akitoa maoni juu ya ubinafsi ulivyoenea, Bwana Wang ameusihi ulimwengu "usikae kimya tu." Kwa kutambua jukumu muhimu ambao Mkataba wa Kikosi cha Nyuklia cha Kati (INF) unalichukua katika kudumisha urari wa kimkakati na utulivu, kujiondoa katika umoja kunaweza kusababisha athari nyingi mbaya.”

Amesisitiza kwamba "China inapingana kupelekwa kwa makombora ya masafa ya kati katika eneo la Asia Pasifiki," na kwamba "Uchina itaendelea kushiriki katika mchakato wa kimataifa wa kudhibiti silaha."

Pia amezungumzia mada zingine kubwa kama vile suala la nyuklia la Irani, na kuitaka"irejee haraka kufuatilia mkakati wa JCPOA (Mpango Kabambe wa kuchukua hatua)."

Amesema kwamba nchi za Ghuba zinapaswa kuhimizwa kutekeleza mazungumzo na mashauriano, na nchi kutoka nje yaeneo hilo zinapaswa "kuchukua jukumu nzuri katika kudumisha usalama katika eneo hilo."

Akigeukia rasi ya Korea, Bwana Wang amesema fursa ya suluhu ya kisiasa haipaswi kupigwa tena.

"Ni lazima kwa Baraza la Usalama kuzingatia kurejelea sheria za kurudisha nyuma ya maazimio ya kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea ili kuunga mkono azimio la kisiasa kuhusu rasi ya Korea”.

Na kuhusu Myanmar na Bangladesh Bwana. Wang amesema juhudi za upatanishi za Uchina zimesaidia nchi hizo mbili kufikia maelewano mapya kuhusu kurejea wakimbizi wa Rohingya. “Hatua Dhahiri ndizo zitakazorejesha matumaini na kuweka mazingira ya kufikia muafaka wa mwisho kuhusu suala la Rakhine.”