Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simama kidete sasa kupigania haki za wazee:UN

Bibi anasaidiwa kutembea ili afike kwenye kibanda cha kupiga kura mnamo 2006, huko Port-au-Prince, na afisa wa polisi wa Umoja wa Mataifa.
UN Photo/Sophia Paris
Bibi anasaidiwa kutembea ili afike kwenye kibanda cha kupiga kura mnamo 2006, huko Port-au-Prince, na afisa wa polisi wa Umoja wa Mataifa.

Simama kidete sasa kupigania haki za wazee:UN

Haki za binadamu

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wazee ambayo kila mwaka huadhimishwa Oktoba Mosi, mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu wazee kufurahia haki zote za binadamu ametoa wito kwa kila mtu kusimama kidete kwa ajili ya kuhakikisha haki za wazee zinatimizwa.

Mtaalam huyo Rosa Kornfeld- Matte kupitia taarifa yake iliyotolewa leo amesema, “leo hii wazee tofauti na ilivyo wanawake, watoto, watu wenye ulemavu, wahamiaji au wakimbizi wanalindwi na chombo chochote cha kimataifa cha haki za binadamu. Mfumo wa kisheria wenye mahitaji maalum ya wazee sawa namakundi mingine katika wakati mgumu hivi sasa haupo.”

Ameongeza kuwa kukosekana kwa chombo maalum cha kisheria kwa ajili ya wazee ndiko kunakoeleza pia ukosefu wa kupewa kipaumbele kwa changamoto maalum zinazowakabili wazee , wake kwa waumme katika mfumo wa sera za kimataifa ikiwemo malengo ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatoa muongozo wa hatua za Umoja wa Mataifa mashinani.

Amesisitiza kwamba “Ni muhimu mfumo wa utekelezaji wa SDGs ukazingatia misingi ya kawaida ili kuhakikisha ujumuishwani na uendelevu utakaoleta ufanisi wa muda mrefu.”

Amesema katika zama hizi za mabadiliko kukiwa marambili idadi ya watu wa umri wa kati ya miaka 55 na zaidi hadi kufikia takribani bilioni 2, hatua za haraka zinahitajika . “Tunahitaji kusimama imara kupigania haki za wazee. Nasikitika kwamba kunaonekana hakuna ari ya haraka , sauti za kupiga debe la kupitishwa mtazamo wa kuzingatia haki za binadamu za kuelekea uzee , kubalidi mwelekeo wa jamii hadi kwa wazee wenyewe hakusikilizwi licha ya ukweli na takwimu zilizopo hali inayofanya watu watafakari ingawa tunapenda kuishi kwa muda mrefu iwezekanavvyo hatutaki kuzeeka.”

Kauli mbiu yam waka huu ni “Safari ya usawa wa umri” nan chi zina wajibu wa kuchagiza na kulinda haki za binadamu za wazee.