Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tusidhalilishane mitandaoni bali tuelimishane-Ogola 

Balozi mwema wa wakfu wa Umoja wa Mataifa au UN Foundation Philip Ogola.
UN News/Patrick Newman
Balozi mwema wa wakfu wa Umoja wa Mataifa au UN Foundation Philip Ogola.

Vijana tusidhalilishane mitandaoni bali tuelimishane-Ogola 

Msaada wa Kibinadamu

Mitandao ya kijamii ina hatari na athri kubwa zaidi kwa vijana inapotumiwa vibaya amesema balozi mwema wa wakfu wa Umoja wa Mataifa au UN Foundation Philip Ogola.

Akizungumza na Flora Nducha kandoni mwa mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini New York kijana Ogola amesema wanachokifanya mabalozi wema 14 wa wakfu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadu na mtandao ni kuelimsha vijana kutumia vyema mitandao kwa faida za maendeleo na wazazi kuwa karibu na vijana wao kwani wao ni sehemu ya tatizo.Lakini kwa nini vijana wanageukia mtandao badala ya wazazi, Ogola anasema, "unajua kama sisi enzi zetu hatukuwa na mtandao sasa unapata vijana wengi sasa hivi wa enzi za kisasa hawana upendo nyumbani. Kwa hiyo upendo wanapata kwenye mtandao. Kwangu  mimi shida kubwa hasa as a digital humanitarian tumeona tukienda kwa vikao vya shule, vijana wengi wantuambia wazazi hawa.....mzazi anakuja nyumbani amechelewa wakiwa na changamoto wakiuliza wazazi mzazi anasema.... eee usinisumbue. Kwa hiyo kuna vijana wengi wanaenda kupata malezi bora kwenye mtandao, na hio pale kwenye mtandao kuna wakora kuna watu wanakutusi kuna mtu wa... watu hawajali wananyanyaswa wanatukanwa na hawana mtu wa kuwaelekeza juu mzazi hayuko nyumbani."

Changamoto kubwa kwa vijana ni kunyanyaswa kwa mtandao ambapo Ogola amependekeza wazazi washiriki katika kuelewa wanayoyapitia vijana kwenye mtandao kwani mitandao ya kijamii inatumika vibaya na udhalilishaji wa wanaopitia ni mkubwa kiasi cha kutojua jinsi ya kukabiliana nao.