Nchi 38 zinazoendelea za visiwa vidogo, ni kati ya nchi zilizo hatarini zaidi

29 Septemba 2019

Nchi 38 zilizotambuliwa na Umoja wa Mataifa kama nchi zinazoendelea za visiwa vidogo, au SIDS, ni kati ya nchi zilizo hatarini zaidi ulimwenguni. Nchi hizi ambazo ziko kwenye eneo la Karibea, bahari ya Pasifiki, ya Atlantiki, ya Hindi na Bahari ya Uchina ya Kusini zinaathirika na hali inayozidi ya mabadiliko ya tabianchi ulimwenguni ambayo haitabiriki. Pamoja na changamoto za mazingira, SIDS inakabiliwa na seti ya kipekee ya masuala yanayohusiana na udogo na umbali.

Mataifa mengi ya visiwa huwa yanakabiliana na vizuizi vivyo hivyo katika juhudi zao za kujikuza kiendelevu, kama vile msingi mdogo wa rasilimali, masoko madogo na utegemezi mzito kwa masoko machache ya nje wakati mwingine. Pia kwa ujumla wanakabiliwa na gharama kubwa za vyakula, ambavyo mara nyingi lazima viingizwe kutoka nje, pamoja na nishati, miundombinu, usafirishaji na mawasiliano. Changamoto hizo zinakanganya zaidi kutokana na shida zinazokumbana nazo kuhamasisha fedha za maendeleo kwa masharti nafuu na sahihi.

SIDS zinaathiriwaje hivi sasa?

UN Photo/OCHA/Mark Garten
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alipotembelea Kisiwa cha Abaco, Bahamas kushuhudia uharibifu uliosababishwa na Kimbunga Dorian. Picha ya Umoja wa Mataifa / OCHA / Mark Garten

Bi 'Utoikamanu akiongea na UN News kuhusu changamoto zinazokabili SIDS asema “mnamo Mei mwaka wa 2019, Katibu Mkuu alitembelea Tuvalu na kusema kwamba kuongezeka kwa kiwango cha bahari katika nchi zingine za Pasifiki kimezidi wastani wa ulimwengu na kwamba ni tishio kwa nchi kadhaa za kisiwa. Mishtuko ya tabianchi na upangaji wa kipekee wa SIDS inafanya iwe vigumu kukuza kwa mtindo endelevu na kuboresha maisha ya raia wao”

Hii inauhusu vipi ulimwengu wote ... hii si ni shida ambayo SIDS inahitaji kushughulikia?

 

UNDP Tuvalu/Aurélia Rusek
Tuvalu, moja ya visiwa vya Bahari ya Pacific vikiwa kwa wastani chini ya mita mbili juu ya usawa wa bahari. Hali hii imetokana na mabadiliko ya tabia nchi.

SIDS ni nchi zinazoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi lakini kwa kuzingatia kwamba kwa ujumla zinatoa gesi ndogo chafuzi ambazo zinasababisha mabadiliko ya tabianchi, pia ni nchi ambazo hajisababisha janga hili kwa ukubwa. Kwa hivyo, mataifa yote, haswa yenye viwanda ambayo yametoa gesi nyingi zenye hatari, wana jukumu la maadili la kuchukua hatua.

Athari hii inadhihirika kote ulimwenguni katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea. Kwa hivyo, ni suala la ulimwenguni kote ambalo linagusa watu kila mahali.

Kwa hivyo ni masuluhisho gani yanayopatikana?

Changamoto kubwa inayowakabili nchi ndogo zinazoendelea za visiwa vidogo ni suala la tabianchi, hivyo, zinahitaji kuenenda na tishio jipya, na kutafuta njia za kujikuza kiendelevu. Zinanahitaji kujenga uimara wa kiuchumi na mazingira.

SIDS zinajitokeza kama vitangulizi katika harakati za kutafuta mifumo ya nishati mbadala kuendeleza matumizi ya rasilimali ya asili. Ingawa zina mchango mdogo katika uzalishaji wa gesi chafu, zinatambua kuwa zinaweza kuwa mifano kwa ulimwengu wote.

Kwa mfano, katika kisiwa cha Comoro, Bahari ya Hindi, wakulima wanabadili njia za ukulima kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya tabianchi kama vile ongezeko la joto na upungufu wa mvua.

UNDP/Andrea Egan
Mtunzaji wa uhifadhi wa eneo hili Alfred Masul anarudi kupanda miti ya mikoko huko Papua New Guinea ili kujenga sitahamala dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. UNDP / Andrea Egan

Jijini Papua New Guinea, mtunzaji wa mazingira wa ndani Alfred Masul anafanya kazi ya kujenga mnepo wa hali ya hewa kali na kuongezeka kwa viwango vya bahari. Yeye analinda pwani dhaifu ya nyumba yake ya kisiwa kwa kupanda miti ya mikoko, ambayo pia itafanya samaki kurudi kwenye maji ya ndani na kuwa chanzo muhimu cha chakula.

Nchini Jamaica, huko Karibea, ambayo imekuwa ikiteseka na ukame siku za hivi karibuni kufuatia kupungua kwa mvua kwa asilimia 30, jamii zinajifunza kuvuna maji ya mvua, zoezi ambalo linaweza kuleta utulivu na kusaidia kuleta maendeleo kwa kufanikisha usalama wa chakula na kuunda ajira.

SIDS zitatumaini kulenga nini New York mwezi huu?

Jumuiya ya kimataifa itajiunga na nchi zinazoendelea za visiwa vidogo katika mkutano wa ngazi ya juu katika Umoja wa Mataifa jijini New York ili kukagua jinsi SIDS zinavyokuza maendeleo endelevu huku zikikabiliwa na hali ya sasa ya tabianchi. Watazingatia zana kuu, SAMOA Pathway, maelezo ya maendeleo endelevu kwa nchi za visiwa ambayo yalikubaliwa miaka mitano iliyopita katika mji mkuu wa nchi ya Bahari ya Pasifiki.

Inatarajiwa kuwa hatua mpya zitachukuliwa katika hatua za tabianchi, kwamba bahari zinazozunguka visiwa zinaweza kuhifadhiwa vyema na mifumo ya afya ya umma inaweza kuimarishwa. SIDS pia zitaangalia kuongeza fursa mpya za ukuaji wa uchumi na vile vile kukuza maendeleo endelevu kwa kuunda ushirika wa kweli na wa kudumu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud