Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwa na akiba ya fedha kwenye simu hakuna maana kama huwekezi- Dkt. Kituyi

Katibu Mkuu wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi
UN News/Grece Kaneiya
Katibu Mkuu wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi

Kuwa na akiba ya fedha kwenye simu hakuna maana kama huwekezi- Dkt. Kituyi

Ukuaji wa Kiuchumi

Katibu Mkuu wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi amesema teknolojia ya kuwa na fedha kwenye mtandao wa simu hadi mashinani itakuwa na maana zaidi pale watu watatumia fedha hizo kujiongezea kipato. 

Akizungumza nami kando mwa kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74, kuhusu ufadhili kwa maendeleo jijini New York, Marekani, Dkt. Kituyi amesema ,“uwezekano wa kuwa na pesa kwenye simu ni tofauti na kuwa na pesa. Ni kwamba teknolojia ya kidijitali inawezesha sasa hata mtu wa mapato madogo akawa na mbin uza kuweka na kutumia fedha, lakini huweiz kueneleza faida hiyo bila ya kuwekeza kwenye mapato, na zile mbinu za kutengeneza fedha ndio utumie fedha , sasa lazima  ajue kwamba hiyo ni fursa sasa ya kufanya biashara aendeleze kuwekeza kwenye mapato ili kutumia fursa hiyo iwe ya maana, aende kutafuta soko mpya, kuna mbinu mbalimbali za soko la bidhaa zako. Mama mzee nyumbani sasa anaweza kuopata malipo ya maziwa na mazao yake bila akaunti ya mume wake. Hii ni mbinu ya kulipa na kulipwa sasa ni changamoto ni kuendeleza mapato ili ulipwe kupitia mbinu hiyo.

Nikamuuliza Dkt. Kituyi ina maana urahisi huu wa malipo ya haraka kupitia simu ya mkononi una hatari yoyote?,“urahisi wa kutumia fedha kwa sababu ya simu ya mkononi umeanza kudhuru wengine ambao wameingia kwenye michezo ya kamari kama unaenda Kenya hivi sasa wanaume wengi wanakopa fedha ili kucheza kamari wanafikiria ni uwekezaji, sasa familia nyingi zinafilisika kwa sababu teknolojia imewezesha watu kupoteza, sasa kutahadhari kuwa urahisi wa kutoa fedha si mfano wa kuendelea, unakuwa fursa na unaweza kuja na changamoto nyingine.”