Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili wa SDGs na mabadiliko ya tabianchi unademadema:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi
UN Photo/Cia Pak
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Ufadhili wa SDGs na mabadiliko ya tabianchi unademadema:UN

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya mbele ya mjadala mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba kuna pengo kubwa la ufadhili ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs na kukabiliana na dharura ya mabadiliko ya tabianchi.

Antonio Guterres amewaambia nchi wanachama waliohudhuria mkutano hu oleo kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani kwamba “Hatuko katika msitari unaotakiwa kufikia SDGs, tuko nyuma katika ukusanyaji wa fedha za ufadhili tunazohitajiiwe katika sekta ya umma au binafsi, hii ndio changamoto yetu kubwa katika kutimiza ajenda ya 2030.”

Katika mkutano huo uliowaleta pamoja viongozi wa serikali mbalimbali, sekta za biashara na sekta za fedha , Katibu Mkuu amesema “Kupungua kwa msaada wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo na kuongezeka kwa mzigo wa madeni ya kupita kiwango katika matumizi ya SDGs kunaongeza hatari. Karibu Theluthi moja  ya nchi zilizo na maendeleo duni ulimwenguni hivi sasa zinaishi katika hali ya madeni ya kupindukia au ziko katika hatari. Hali hiyo pia inaleta hofu katika mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea ambazo zinamzigo mkubwa wa madeni huku zikikabiliwa na gharama zingine za uharibifu uliosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi. Licha ya Habari hizo mbaya kuna Habari za kutia matumaini ambayo yanatupa sababu ya kuendelea kuamini n anchi kuchukua hatua ”

Amesema masoko ya fecha hivi sasa zaidi na zaidi yanajumuisha uendelevu katika mfumo wa kuendesha biashara. Wawekezaji, wanaotoa bima na masoko ya hisa wamepitisha mipango ya kanuni za uwajibikaji na uendelevu.

Mapema wiki hii kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa taasisi za benk walipitisha kanuni za uwajibikaji wa Benki na kuahidi dola trilion 35kusaidia masuala ya utekelezaji wa SDGs. Guterres amekumbusha kwajibu wa kuyaweka malengo ya maendeleo endelevu kuwa kipaumbele na si ndoto tena”Hii inamaanisha kuvuka vikwazo kwa ajili ya ufadhili wa muda mrefu  na kuichagiza sekta ya fecha kuorodhesha hatari zote za hulka zisizoendelevu.”

Kisha akasema ni muhimu kuzisaidia nchi kukusanya rasilimali zake za kitaifa kuweza kugharamia mikakati ya utekelezaji wa maendeleo endelevu.

Kukabiliana na kutohusishwa na huduma za kifedha

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia ametoa wito wa kukabiliana na hali ya kutojumuishwa hatika huduma za kifedha ambako kumeathiri watu wengi . ametoa wito wa kuunda kikosi kazi kutathimini jinsi gani kuingiza mfumo wa fecha katika masuala ya kidijitali kunaweza kusaidia kuchagiza ujumuishwaji  na maendeleo endelevu.

wanawake ni lazima wake katika kitovu cha ujumuishwaji hususan wanawake masikini , wanawake wajasiriamali na wanawake wanaoendesha familia zao .”

Ameongeza kuwa nchi zenye maendeleo dunia ambazo ufadhili binafsi ndio ulio chini kuliko kwingineko pia ni kwa kupewa kipaumbele.

Na mwisho amesisitiza kwamba ushirikiano wa kimataifa ndio kiini.”Ushirikiano ni muhimu kupambana na masuala ya kukwepa kodi na ubadhilifu, ufisadi na mifumo haramu ya fecha masuala ambayo yanazinyima nchi zinazoendelea mabilioni ya dola ambazo ni rasilimali kwa ajili ya maendeleo yao kila mwaka” Ushirikiano huu pia utakuwa muhimu na wa lazima kukabiliana na changamoto ya kodi katika uchumi huu wa kidijitali.”