Umoja wa Mataifa wazindua mikakati ya kuzuia unyanyasaji kingono na kuuzwa watoto

Umoja wa Mataifa wazindua mikakati ya kuzuia unyanyasaji kingono na kuuzwa watoto
Kamati ya Umoja wa Mataifa ambayo inafutilia haki za watoto inazinduliwa rasmi leo Alhamisi ikiwa na malengo ya kusaidia nchi kutekekeza makubaliano yanayohusu kuuzwa kwa watoto, watoto kutumiwa katika umalaya na biashara ya picha za uchi za watoto.
Maelekezo hayo yaliandikwa na Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za mtoto inaangazia sana vitisho vipya vinavyowalenga watoto kote duniani kutonana na teknolojia ya kidijitali kama intaneti na mitandao ya kijamii.
Kuboreka kwa teknolojia ya mawasiliano imewapa fursa mpya wanyanyasaji wa kimapenzi na njia za kuwadhulumu watoto. Zinatumiwa kuwavutia watoto kujiunga katika masuala ya ngono kwa njia ya video zinazotangazwa moja kwa moja mitandaoni.
Waendesha uovu huo huwasiliana na kubadilishana habari huku wakitumia mitandao ya siri kutekeleza vitendo hivyo.
Hii imekuwa changamoto mpya na ngumu kwa idara za sheria. Katika ulimwengu ambao matumizi ya mitandao ni kitu kinazidi kukua kwa kasi, tisho la watoto kunyanyaswa kingono au kununuliwa na kuuuzwa kama bidhaa ndani ya nchi ni nje imekuwa ikiongezeka kwa kasi sana.
Miongozo hiyo ina lengo la kuleta uelewa zaidi wa mpango huo wa Umoja wa Mataifa na kutoa suluhu mwafaka kuambatana na changamoto ambazo nchi zimekabiliana nazo katika utekelezwaji wake.
Inalenga kusaidia nchi 176 ambazo zimetia sahihi mpangilio huo na pia zile zitakazojiunga nao baadaye.