Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila ufadhili zaidi, mwezi Oktoba tutalazimika kupunguza mgao wa chakula Yemen-WFP

Wafanyakazi wakipanga msaada wa chakula katika nyumba ya hifadhi Lahj, Yemen. (Julai 1 2019)
WFP/Saleh Baholis
Wafanyakazi wakipanga msaada wa chakula katika nyumba ya hifadhi Lahj, Yemen. (Julai 1 2019)

Bila ufadhili zaidi, mwezi Oktoba tutalazimika kupunguza mgao wa chakula Yemen-WFP

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP nchini Yemen limesema linakabiliwa na upungufu mkubwa wa ufadhili na linahitaji dola milioni 600 ili liweze kuendelea na msaada wa chakula kwa miezi sita ijayo.

 

WFP imesema bila ufadhili zaidi itakuwa haina namna nyingine isipokuwa kupunguza mgao wa chakula kwa familia zenye uhitaji kuanzia mwezi ujao wa Oktoba.

“Mtiririko endelevu wa chakula kuingia Yemen ni wa muhimu  kuhakikisha kuwa msaada unaohitajika sana na mamilioni ya watu wenye njaa unawasilishwa kila mwezi,” imeeeleza taarifa ya WFP iliyotolewa leo mjini Sana'a nchini Yemen.

WFP imesema kwa mwezi Agosti ilifikia rekodi ya juu ya usambazaji wa chakula kwa watu milino 12.4. Yemen ni eneo gumu na tata kwa wasambazaji huduma ingawa WFP imeendelea kuongeza msaada kote nchini humo ili kuzuia kuongezeka kwa hali ya ukosekanaji wa chakula.

Aidha ili kupambana na vyakula kufika katika mikono ya wasio walengwa, WFP inafanya usajili wa watu wenye uhitaji wa chakula kwa njia ya mashine za kielektroniki.