Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanasayansi wa bahari na mashirika yasiyo ya serikali wataka hatua za kulinda bahari

Msichana kutoka jamii ya Iñupia akiwa bahari ya Arctic ambapo kunashuhudiwa kuyeyuka kwa bahari.
UNICEF/Vlad Sokhin
Msichana kutoka jamii ya Iñupia akiwa bahari ya Arctic ambapo kunashuhudiwa kuyeyuka kwa bahari.

Wanasayansi wa bahari na mashirika yasiyo ya serikali wataka hatua za kulinda bahari

Tabianchi na mazingira

Ripoti maalum ya Jopo la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, IPCCC ikiangazia hali ya bahari na sehemu zenye theluji  imefichua kiwango cha janga linalowakodolea binadamu wakati bahari zinaanza kuonesha dalili za kuporomoka.

Licha ya kuwa bahari na tabianchi ni vitu viwili vinavyoshirikiana kuifanya dunia salama kuishi, hii ndiyo mara ya kwanza jopo hilo limeegemea sana upande wa bahari.

Ripoti hiyo inaeleza kile wanasayasni wa masuala ya bahari na mashirika yasiyo wa serikali  wamekuwa wakisema kwa miaka mingi kuwa bahari inazidi kudorora kutokana na shughuli zikiwemo uvuvi kupita kiasi, uchafuzi na mabadiliko ya tabia nchi.

"Hii dunia ni bahari, ambayo maisha yake yanaendeshwa na bahari moja lakini bahari yenyewe sasa inakumbwa na changamoto zikiwemo kuongezeka kwa joto na uchafuzi unatokana na kemikali. Kile tunataka sasa ni kujitolea kuchukua hatua kulinda bahari kwa manufaa ya binadamu, amesema Profesa Dan Laffoley kutoka tume inayohusika na kutunza maeneo yanayolindwa

Zile hatua zinazochukuliwa kwa sasa ina maana kuwa mabadiliko ambayo tayari yapo yatasalia kwa mamia ya miaka na kwamba licha ya hatua za haraka za kuzuia kupanda viwango vya joto na kupunguza gesi chafu bahari bado zitakuwa katika hatari.

Kati ya sasa na mwisho wa mwaka 2020 maeneo ya bahari ya bahari kuu ambayo hayamilikiwi na nchi yoyote ambayo ni nusu ya dunia yatastahili kulindwa chini ya sheria ya kimataifa. Mkataba mpya unajadiliwa katika Umoja wa Mataifa na nchi zinastahili kukamilisha suala hili mwaka 2020 kulinganana na azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kuzuia kuongezeka joto kwa nyusi joto 1.5 ni muhimu katika kulinda mazingira ya bahari ambapo mataifa yote yanastahili kujitolea katika mipango yote mipya ili kufanikisha hili.