Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nitatumia tuzo na nafasi yangu kuwezesha wanafunzi na jamii- Mwalimu Tabichi

Peter Tabichi wa Kenya, mshindi wa Tuzo ya kimataifa ya Mwalimu. Tabichi ni mwalimu wa sayansi ambaye anatoa asilimia 80 ya mshahara wake kusaidia watu maskini katika shule za vijijini Kenya
UN News/Grece Kaneiya

Utamaduni na Elimu

Lengo langu kama mwalimu ni kuhakikisha kwamba nawawezesha wanafunzi wangu kielimu lakini zaidi nje ya darasa kwa ajili ya kuhakisha wanabobea si tu katika mazingira ya darasa lakini pia kimaisha.

Ni kauli ya mwalimu Peter Tabichi, mshindi wa tuzo ya mwalimu bora kimataifa ambaye alitunukiwa tuzo hiyo kufuatia kujitolea kwake kwa hali na mali katika kufanikisha utendaji wa wanafunzi wake katika shule ya sekondari ya Keriko iliyoko kaunti ya Nakuru nchini Kenya. Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani Mwalimu Tabichi amesema, 

(Sauti ya Mwalimu Peter Tabichi)

Lakini ukarimu wa mwalimu Tabichi umeendelea hata baada ya tuzo ambapo amesema atatumia fedha alizopokea kuimarisha elimu na jamii hapo mashinani

(Sauti ya Mwalimu Peter Tabichi)