Visa visivyothibitishwa vya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania

24 Septemba 2019

Tarehe 10 Septemba 2019 wakati wa shughuli zake za kawaida, WHO ilijulishwa kuhusu ripoti zisizo rasmi kuhusu kifo cha mtu mmoja kutoka na kile kinachoshukiwa kuwa ugonjwa wa Ebola mjini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Ripoti zingine zisizo rasmi zinasema kuwa wale walioshukiwa kukaribiana na mtu huyo waliripotiwa kutengwa katika sehemu tofauti za nchi.

Licha ya maombi kadhaa, WHO hadi sasa haijapokea taarifa kamili zinazohitajika kufahamu hatari iliyopo kutokana na kisa hiki.

WHO na washirika wanaendelea kuwasiliana na mamlaka na WHO iko tayari kuoa utaalamu na msaada mwingine kwa Tanzania, katika kushughulikia hatua yoyote ya dharura ya kiafya ambayo Tanzania inaweza kukabiliwa nayo.

WHO inashauri kusiwe na marufuku yoyoye ya usafiri kwenda nchini Tanzania kutoka na hali hiyo.

Wajibu wa WHO ni kuwajulisha wanachama kuhusu masuala yanayozua wasiwasi na kusaidia nchi kuhusu dharura zozote za afya. Tunataka kuhakikisha tunatekeleza majukumu haya na kusaidia kutoa msaada unaohitajika.

WHO iko katika mawasiliano na mamlaka za afya nchini Tanzania katika viwango vyote kuanzia Geneva, ofisi wa WHO kanda ya Afrika kupitia ofisi ya WHO nchini Tanzania.

Kuanzia kutimika chanjo mpya ya J&J nchini DRC

Jana mamlaka za afya nchini DRC zimetangaza mipango ya kuanza kwa majaribo ya pili ya chanjo ya ugonjwa wa Ebola, iliyotengenezwa na kampuni ya Johnson & Johnson kuanzia kati kati mwa mwezi Oktoba.

Chanjo hii ambayo itatolewa mara mbili kati ya muda wa siku 56 ni kutokana na mipango iliyoidhinishwa kwa maeneo ambayo haswa hayana visa vya maambukizi ya Ebola kama njia ya kuweka kinga dhidi ya maradhi hayo.

Chanjo hiyo ya Johnson & Johnson itatumika sambamba na chanjo ya sasa inayojulikana kama (rVSV-ZEBOV-GP, inayotengenezwa na kampuni  ya Merck), ambayo imetajwa kuwa bora na salama ambayo imesaidia kuokoa maisha ya maelfu ya watu.

Chanjo ya Merck itaendelea kutolewa kwa watu wote walio katika hatari ya juu ya kuambukizwa ugonjwa wa Ebola, wakiwa wale ambao walikaribiana na mtu aliyethibitishwa kuugua Ebola. Hadi sasa zaidi ya watu 223,000 wamepata chanjo hii katika kipindi cha sasa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter