Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya bora huwapa watu utu na matumaini na ndivyo tufanyavyo Rwanda:Kagame

Rais Paul Kagame kutoka Rwanda akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa kongamano kuhusu afya kwa wote.
UN Photo/Kim Haughton
Rais Paul Kagame kutoka Rwanda akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa kongamano kuhusu afya kwa wote.

Afya bora huwapa watu utu na matumaini na ndivyo tufanyavyo Rwanda:Kagame

Afya

Afya bora huwapa watu ut una kuwawezesha kufikia kilele cha mafanikio yao kwani ndio msingi wa maendeleo katika jamii.

Hayo ameyasema Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza leo kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu huduma za afya kwa wote UHC, uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.

Rais Kagame amesisitiza kwamba “Hakuna mzazi anayestahili kuchagua biana ya chakula na dawa kwa familia yake. Kwa mantiki hiyo leo tunarejea ahadi yetu ya kuhakikisha huduma nafuu kwa wote , ubunifu , ukusanyaji wa rasirimali za ndani na ushirikiano wa kimataifa ni mikakati muhimu katika kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa kila mtu.”

Amesema Rwanda haipigi kelele tu bali inazungumza kwa vitendo akitaja mambo matatu makubwa wanayotekeleza ambayo ni “Mosi tumepanua wigo wa wahuduma wa afya wa kijamii kutoka wawili hadi kufikia wanne kila kijiji ambao ni sawa na muhudumu mmoja kwa kila kaya 40 wakisaidia kuhakikisha hakuna anayesalia nyuma, Pili ili kuongeza ufanisi Rwanda imeweka lengo la kuhakikisha kwamba mgonjwa hatembei umbali wa zaidi ya dakika 25 kwenye kupata huduma za afya na hiki ndio kiwango na kazi inaendelea, tatuasilimia 93 ya wasichana wenye umri wa umri wa chini ya miaka 13 Rwanda wamepatiwa chanjo dhidi ya vurusi vinavyosababisha saratani HPV, na hii inadhihirisha umuhimu wa kuongeza ufanisi na pi ahaja ya kujumuisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza katika mkakati wa afya kama vile magonjwa ya saranani ya shingo ya uzazi.”

Ameongeza kuwa bima ya afya ni msingi wa mkakati wa será zao na zaidi ya asilimia 90 ya watu wote nchini Rwanda sasa wana bima ya afya kupitia mipango ya bima ya kijamii na ya sekta binafsi. Pamoja na mafanikio yote hayo Rais Kagame amesema bado kuna changamoto ya kufikia huduma za afya kwa wote kwa asilimia mia moja. Na hilo amesema ni jukumu la kila mmoja aliyeko kwenye mkutano na serikali yake kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja na kuacha kitu ambacho daima kitakumbukwa na hata vizazi, vijavyo ambacho ni huduma ya afya kwa wote.