Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi ziwekeze asilimia 1 katika huduma za afya kwa wote, WHO

Mkurugenzi mkuu wa WHO Adhanom Ghebreyesus alipozuru Butembo nchini DRC Aprili mwaka 2019 baada ya watu wenye silaha kushambulia kituo cha Ebola
WHO/Junior Kannah
Mkurugenzi mkuu wa WHO Adhanom Ghebreyesus alipozuru Butembo nchini DRC Aprili mwaka 2019 baada ya watu wenye silaha kushambulia kituo cha Ebola

Nchi ziwekeze asilimia 1 katika huduma za afya kwa wote, WHO

Afya

Nchi ni lazima ziongeze matumizi kwenye huduma za kimsingi za afya kwa takriban asiliamia 1 ya pato loa la kitaifa ikiwa dunia inataka kupunguza mianya ya kutimiza malengo ya afya ifikapo mwaka 2015,  kwa mujibu wa ripoti mpya kutoka kwa Shirika la Afya Duniani na washirika kabla ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa huduma za afya zilizo muhimu.

Dunia inahitaji kuongeza mara dufu utoaji huduma muhimu za afya kati ya sasa na mwaka 203 kwa mujibu wa ripoti hiyo. Inaonya kuwa ikiwa hali ya sasa itaendelea adi watu bilioni 5 bado hawatakuwa na uwezo ya kupata huduma hiyio ifikapo mwaka 2030 ukiwa ndio mwaka wa mwisho uliowekwa na viongozi wa dunia wa kuwepo huduma muhimu za afya kwa watu. Wengi wa watu hao ni maskini.

“Ikiwa kweli tunataka kutimiza lengo la huduma ya afya kwa wote na kuboresha maisha ya watu, ni lazima tutimize kwanza afya ya msingi, anasema Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkugenzi mkuu wa WHO.

 Kuwekeza dola bilioni 200 zaidi kila mwaka katika koboresha huduma za kimsingi za afya kwa nchi maskini na zile la kipato cha wastani inaweza kukoa kwa kiwango kikubwa maisha ya watu milioni 60, iongeze miaka ya kuishi kwa miaka 3.7 ifikapo mwaka 2030 na kuchangia sana maendelea ya kijamii na kiuchumi.

Asilimia kubwa ya ufadhili utakuwa ndani ya nchi zenyewe. Ripoti hiyo inasema nchi nyingi zinaweza kuongeza huduma za msingi za afya kwa kutumia raslimali za ndani –labda kwa kuongeza matumii katika sekta ya afya kwa jumla au kwa kuelekeza matumizi kwa afya au kwa kufanya vyote.

Nchi ni lazima ziongeze nguvu za utoaji huduma kote katika nchi zao. Licha ya kwamba utaoji huduma umeongezeka tangu mwaka 200, hatua zimepungua kasi  miaka ya hivi karibuni. Ongezeko limeshuhudiwa katika za kipato cha chini lakini bado zimasalia nyuma.

Wanawake wengi sana na watoto wanaendelea kufa kutokana na magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa njia rahisi kwa sababu hawezi kupata huduma wanayohitaji ili kuishi alisema Henrieta Fore mkurugenzi wa UNICEF.

Watu wengi wanatabika kutokana na athari za kulipiia huduma kutoka kwa mifuko yao kuliko miaka 15 iliyopita. Karibu watu milioni 925 hutumia zaidi ya  asilimia 10 ya kipato chao kwa huduma za afya huku milioni 200 wakitumia asilimia 25 ya kipato chao.

Ni jambo la kushangaza kuona watu wakiwa  na wakati mgumu kupata mahitaji yao kwa sababu wanalipia saana huduma zao za afya hata kwenye nchi zilizostawi, anaongeza Angel Gurria katibu mkuu wa OECD.