Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takriban watu milioni 72 duniani wanahitaji lugha za ishara ili kutimiza SDGs:UN

Mkalimani wa lugha ya ishara akiueleze afunguzi wa mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri kuhusu maendeleo endelevu (17 Julai 2017)
UN Photo/Manuel Elías
Mkalimani wa lugha ya ishara akiueleze afunguzi wa mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri kuhusu maendeleo endelevu (17 Julai 2017)

Takriban watu milioni 72 duniani wanahitaji lugha za ishara ili kutimiza SDGs:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo ni siku ya kimataifa ya lugha za ishara ambayo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni muhimu sana kuhakikisha takrikutomwacha yeyote nyuma.ban watu milioni 72 hawaachwi nyumba na treni ya kutimiza ajenda ya maendeleo ya 2030.

Antonio Guterres katika ujumbe wake maalum amesema siku hii inatambua umuhimu wa lugha ya ishara katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs na kutomwacha yeyote nyuma.

Pia amesema siku hii inatoa fursa kusaidia na kulinda hadhi na utamaduni kwa watumiaji wote wa lugha ya ishara.

Kwa mujibu wa shirikisho la viziwi duniani kuna takribani watu milioni 72 ambao ni viziwi kote duniani. Zaidi ya asilimia 80 wanaishi katika nchi zinazoendelea na kwa pamoja wanatumia lugha za ishara zaidi ya 300.

Mkalimani wa lugha ya ishara akiwa katika mkutano
Centre/Stéphanie Coutrix
Mkalimani wa lugha ya ishara akiwa katika mkutano

 

Lugha za ishara ni lugha za asili  na zenye mfumo tofauti na lugha ya kawaida ya kuongea, na pia kuna lugha ya kimataifa ya ishara ambayo hutumiwa na viziwi katika mikutano ya kimataifa na iliyo rasmi  wanaposafiri na kukutana na watu kutoka sehemu mbalimbali . Inachukuliwa kama kitovu cha lugha ya ishara  ambayo si ngumu sana ingawa ina mipaka.

Guterres amesema mkataba wa haki za watu wenye ulemavu unatambua na kuchagiza matumizi ya lugha la ishara na kuweka bayana kwamba lugha hizo za ishara zina hadhi sawa na lugha ya kawaida ya kuongea na umezitaka serikali kuwajibika kuziwezesha na kusaidia lugha za ishara  ziwezwe kufundishwa na watu kuzitambua ili kuisaidia jamii ya viziwi katika jamii.

Kauli mbiu ya mwaka huu wa 2019 wa siku ya lugha za ishara duniani ni “Haki ya lugha ya ishara kwa wote”.