Katibu Mkuu aelezea wasiwasi wake kufuatia shambulio la Al Hali

21 Septemba 2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameelezea wasiwasi wake kufuatia shambulio la anga la asubuhi ya Ijumaa Septemba 20 mwaka huu wa 2019 katika vitongoji ya wilaya ya Al Hali katika jimbo la Hudaydah, kaskazini mwa bandari la mji wa Hudaydah.

Katibu Mkuu kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake ametoa wito kwa pande husika kujizuia na kuhakikisha kwamba wanazingatia mapendekezo ya makubaliano ya Hudaydah ya Desemba 13 mwaka 2018.

Bwana Guterres amerejelea kwamba pande husika walielezea dhamira yao kusitisha mapigano kwa mujibu wa mapendekezo ya mkataba wakati wa mkutano wao wa pamoja wa kamati ya uratibu mapema mwezi huu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud