Amani sio tu kutokuwepo vita bali pia kujenga mazingira ya utangamano:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (wa nne kushoto) akishiriki tukio la ugongaji wa kengele wakati wa kuadhimisha siku ya amani katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (20 Septemba 2019)
UN Photo/Kim Haughton
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (wa nne kushoto) akishiriki tukio la ugongaji wa kengele wakati wa kuadhimisha siku ya amani katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (20 Septemba 2019)

Amani sio tu kutokuwepo vita bali pia kujenga mazingira ya utangamano:Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres amesema mara nyingi dunia inaiangalia amani katika mtazamo wa migogoro baina ya binadamu. Lakini amani sio tu kutokuwa na vita, ni kutengeneza mazingira ya kuwa na utangamano na utulivu kwa njia ambayo watu wataishi pamoja na kuruhusu vita kutotokea.

Guterres ameyasema hayo leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa akiwa na kundi kubwa la vijana kutoka nchi mbalimbali katika tukio la kuadhimisha siku ya amani duniani ambayo kwa kawaida hufanyika Septemba 21 na kusema, "leo tuna siku ya amani, kwa sababu sio tu kuhusu amani miongoni mwa watu lakini ni kuhusu amani baina ya watu na maliasili. Amani baina ya watu na sayari dunia."

"Ukweli ni kwamba kwa sasa zaidi ya karne moja tumekuwa katika vita na sayari yetu. Tumekuwa tukitukiathiri dunia ambayo tunapaswa kuishi na sayari ambayo nimeishi ndani yake nina umri wa miaka 70, nyie ni wadogo, lakini pia nina wajukuu na ninataka kuhakikisha sayari ambayo wataishi itakuwa japo bora kwa maisha, kwa binadamu kama ilivyo leo hii. Lakini hili halina hakikisho." amesisitiza Bwana Guterres.

Guterres amesisitiza kwamba “tunachokifanya leo hii duniani kinaathiri kwa kiasi kikubwa afya ya mazingira, na afya ya sayariyetu. Tuko katika vita na mazingira na tatizo na mazingira ni kwamba lyanalipiza kisasi Mazingira yamekasirika, mazingira hayasamehi, yanaposhambuliwa , yanashambulia pia.”  Wiki iliyopita nilikuwa visiwa vya Bahama na bila shaka umesikia kwenye vyombo vya Habari kuwa katika moja ya visawa kila kitu kimesambaratishwa na upepo mkali , umeua watu na kuharibu nyumba, kuangusha miti na kila kitu. Mazingira yamekasirika, tunahitaji kuwa na amani na mazingira yetu  na ukweli kwamba hatufanyi juhudi za kuwa na amani na mazingira , na ukweli kwamba mazingira yakekasirika , pia inasababisha migogoro zaidi miongoni mwa watu.

Habari za UN
Siku ya Amani duniani huadhimishwa kila mwaka Septemba 21

Ameongeza kuwa “ukienda ukanda mmoja kwenye baraza la Afrika, Sahel Kusini mwa Jangwa la Sahara utaona kwamba mabadilkiko ya tabianchi yanaongeza ukame na hali ya jangwa. Kuna wakulima na wafugaji ambao wameishi kwa amani kwa karne na karne , lakini sasa kwa sababu ya ukosefu wa maji na malisho wafugaji wamelazimishwa kuondoka kwenye kwenye maeneo ambayo wakulima wana shughuli zao na hii imesababisha sokomoko kubwa miongoni mwa makundi hauyo mawili ya wakulima na wafugaji. Na kwa kuwa wanatoka dini mbalimbali na wakati mwingine makabila mbalimbali hilo nalo linapenyeza  katika mfumo wa machafuko katika kanda hiyo na inachochea kusambaa kwa ugaidi katika eneo la Sahel  ambao ni toishio kubwa kwetu sote , kwa sababu ugaidi kama unavyojua ni zahma ya dunia nzima.”

Hivyo amesema kitu cha muhimu sana leo hii ni kwamba hata kama nchi bado hazina utashi wa kisiasa , hata kama hatuwezi kuwa na mani kamili na mazingira , kuna tumaini kubwa kwa yanayoendelea kufanywa na vijana kote duniani. Na vijana wanawaambia watu wa kizazi changu kwamba tunahitaji kubadili mwenendo  na kutahitaji kufanya hivyo sasa, na wanayasema hayo kwa nguvu zote.

Hivyo “Uongozi wenu vijana ni muhimu sana kuhakikisha kwamba kizazi changu kinafanya yaliyo sahihi na bado kuna vikwazo vingi vya kuvishinda. Ninawategemea na nawatakia kila la heri katika ushiriki wenu kuleta amani miongoni mwa binadamu na amani na asili na mazingira yetu.”