Asili "moja ya njia bora" ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Mkurugenzi mkuu wa UNEP Inger Andersen, akihutubia mkutano mjini Nairobi, Kenya.
UNEP/Cyril Villemain
Mkurugenzi mkuu wa UNEP Inger Andersen, akihutubia mkutano mjini Nairobi, Kenya.

Asili "moja ya njia bora" ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Tabianchi na mazingira

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, UNEP, Inger Andersen,  asili ni "moja ya njia bora" za kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kwamba kila nchi inapaswa kuzingatia asili katika mikakati yao ya tabianchi.

Viongozi wa dunia watakusanyika katika Umoja wa Mataifa mjini New York wiki ijayo kuanzia Jumatatu  Septemba 23 kwenye mkutano wa  tabianchi ambao utasimamiwa na Katibu Mkuu Antonio Guterres. Bi Andersen atakuwepo kuhamasisha wazo la masuluhisho ya kiasili ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

UNEP inaunga mkono moja ya hatua tisa za mkutano zilizotengwa na Katibu Mkuu chini ya uongozi wa Serikali ya China na New Zealand.

Akihojiwa na UN News, Bi Andersen aliulizwa ni jinsi gani asili inavyoweza kusaidia kutokomeza mabadiliko ya tabianchi, amesema kwamba tabianchi ya ulimwengu inabadilika haraka sana na mabadiliko haya yanaonekana katika maisha ya kila siku. Joto la Dunia linaongezeka, taratibu za mvua zinabadilika, baionai inapotea, mizunguko ya kilimo imevurugika na msongo kuhusu maji unakuwa jambo la kawaida.  Majanga ya asili kama vile mafuriko, ukame, vimbunga na jotovinakuwa vikali zaidi na mara kwa mara vinazigharimu nchi mabilioni ya dola na kuharibu makazi, miundombinu na maisha. Janga la tabianchi linatishia ustawi, uhakika wa chakula na kuzidisha umaskini.

Je, suluhisho la njia ya asili ni nini?

Suluhisho la kiasili ni hatua za kulinda, udhibiti endelevu na kurejesha mfumo halisi wa ikolojia ulioboreshwa ambao pia unashughulikia changamoto za kijamii, na hivyo kuleta faida za za ustawi wa kibinadamu na baionuai. Kwa hivyo, iwe ni uhakika wa chakula, mabadiliko ya tabianchi, uhakika wa maji, afya ya binadamu, hatari ya janga au maendeleo ya kiuchumi, maumbile ya asili yanaweza kuchangia kupata njia ya suluhisho.

“Na mabadiliko ya tabianchi ni sehemu muhimu wa utatuzi. Kuna njia nyingi za kushughulikia mabadiliko ya tabianchi lakini moja ambayo ni nzuri na ya haraka ni kutumia ambayo iko mlangoni mwetu mayo ni…asili. Mathalani ni mhimu kukumbuka kuwa ni hewa ya ukaa ambayo ambayo inachangia katika hewa chafuzi ambazo zinasababisha joto duniani.”

Mkutano huu wa tabianchi unaosimamiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa unatoa fursa ya kuangazia suluhisho asili katika kuchukua hatua za tabianchi.

Ni aina gani za masuluhisho zilizopo?

Masuluhisho ya kisaili kwa mabadiliko ya tabianchi yanakuja kutokana na kuimarisha na kurejesha mfumo halisi wa asili wa ikolojia uliopo. Mathalani, miti si tu inaondoa hewa ya ukaa, lakini pia inawakinga wanadamu na matokeo mabaya. Miti iliyopandwa vema inaweza kutumika kama vizuzi vya moto, kupanda miti karibu na Mashamba kunaweza kulinda mazao kutokana na mmomonyoko na mvua kubwa, pia misitu inaweza inaweza kudhibiti mafuriko kutokana na namnainavyofonza maji.

Na masuluhisho haya yanagharimu kiasi gani na yanasaidia kiasi gani?

Bi Andersen anasema, “asili ipo hivi sasa na tunatakiwa kuitumia; hakuna ufumbuzi wa haraka wa kiteknolojia ambao una matokeo kama masuluhisho yanayoweza kufanywa na asili. Kimsingi, masuluhisho haya yanaweza kusaidia kupunguza zaidi ya robo ya upunguzaji wa uchafuzi wa hewa kiwango kinachohitajika ulimwenguni kufikia 2030.”

Maumbile ya asili yanapatikana kwa urahisi na tunapaswa kuyatumia; hakuna marekebisho ya haraka ya kiteknolojia ambayo yana kiwango sawa cha athari kama vile suluhisho za msingi wa asili.

Bila shaka, suluhisho hizi za asili zinaweza kupunguza zaidi ya theluthi ya uzalishaji unaohitajika ulimwenguni ifikapo 2030.

Kuna miradi ya kutosha inayoendelea duniani hivi sasa ili kuleta mabadiliko?

“Tuko katika kipindi cha dharura ya Dunia lakini ni katika kipindi cha hali isiyo ya kawaida. Vijana wadogo wanatutaka tuwajibike na kila wiki serikali mahali fulani duniani inaweka ahadi ya kuchukua hatua dhidi ya tabianchi. Masuluhisoho ya asili yapo kwa haraka, gharama nafuu na yanaweza kuongezwa kulingana na uhitaji.  Na kila nchi duniani inaweza kuchukua hatua.” Anasema Bi Andersen.