Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake na watoto wanaishi zaidi leo hii kuliko awali – WHO/UNICEF

Mama na mwana katika kituo cha kitaifa cha afya kwa ajili ya mama na mtoto, Ulaanbaatar, Mongolia.(Septemba 4, 2015)
UNICEF/Jan Zammit
Mama na mwana katika kituo cha kitaifa cha afya kwa ajili ya mama na mtoto, Ulaanbaatar, Mongolia.(Septemba 4, 2015)

Wanawake na watoto wanaishi zaidi leo hii kuliko awali – WHO/UNICEF

Afya

Wanawake zaidi na watoto wao kwa sasa wanaishi zaidi ya hapo awali kulingana na makadirio mapya ya watoto wanaokufa wakati wa kuzaliwa au kina mama wanaofariki dunia wakati wa kujifungua . Makadirio hayo yametolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la  kuhudumia Watoto duniani UNICEF na Shirika la Afya Duniani WHO.

Kwa mujibu wa mashirika hayo tangu mwaka 2000, vifo vya watoto vimepungua kwa karibu nusu au theluthi moja, sababu kubwa ikiwa ni kuimarika kwa huduma za afya kwa wote.

 

“Katika nchi zinazompa kila mmoja huduma za afya zilizo nafuu, salama na za kiwango cha juu, wanawke na watoto huishi na kunawiri, amesema Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkurugenzi mkuu wa WHO.

Bado makadirio mapya yanaonyesha kuwa watoto milioni 6.2 walio chini ya umri wa miaka 15 walikufa mwaka 2018 na zaidi ya wanawake 290,000 walikufa kutokana na matatizo wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua mwaka 2017.

Dkt Doris Chou  ni kutoka kitengo cha afya ya uzazi na utafiti, WHO

« Kile tunachoshuhudia ni kwamba wanawake bado wanafariki kwa sababu kama vile kuvuja damu wakati wa kujifungua, shinikizo la damu wakati wa kujifungua au maambukizo yatokanayo na ujauzito. Lakini kile ambacho tunashuhudia ni kwamba idadi ya vifo vya wanawake kutokana na magonjwa walionayo tayari vimeongezeka, hii ni hali ijulikanayo kama ahtari zisizo za moja kwa moja za ujauzito na hizi ndizo ngumu zaidi kwa wahudumu wa afya kukabiliana nazo kwa sababu ni ngumu kuzipata na kuzigundua.”

Kwa jumla ya watoto wote waliofariki, milioni 5.3 walifariki wakati wa miaka mitano ya kwanza ya uhai wao huku karibu nusu ya vifo hivyo vikitokea wakati wa mwezi wa kwanza wa kuzaliwa.

Wanawake na watoto wachanga ndio wako kwenye hatari wakati na mara tu baada ya kuzaliwa. Takriban wanawake wajawazito milioni 2.8 na watoto wachanga hufariki kila mwaka au mtoto mmoja kwa kila sekundi 11 wengi kutokana na sabauabu zinazoweza kuzuilika, kwa mujibu wa makadirio mapya.

Watoto hukumbwa na hatari ya juu zaidi ya kufariki wakati wa mwezi wa kwanza hususan ikiwa wamezaliwa mapema sana au wakiwa wadogo sana, wakiwa na matatizo wakati wa kuzaliwa au kama wamepata maambukizi. Thuluthi moja ya vifo hivi hutokea wakati wa siku ya kwanza na karibu robo tatu hutokea wakati wa wikiwa mwaka wiki ya kwanza pekee.

Sehemu tofauti duniani, kuzaliwa ni wakati wa furaha. Lakini pia kwa kila sekunde 11 kuzaliwa kwa mtoto ni mkasa kwa familia, alisema Henrieta Fore, Mkurugenzi mku wa UNICEF.

Ukosefu mkubwa wa usawa duniani

Makadirio pia yanaonyesha ukosefu mkubwa wa usawa kote duniani, huku wanawake na watoto walio kusini mwa jangwa la sahara wakikumbwa na hatari kubwa ya kufariki kuliko sehemu zingine zote.

Viwango vya vifo wakati wa kujifungua viko mara 50 zaidi juu kwa wanawake kusini mwa jangwa la sahara na watoto wao wakiwa mara 10 i ya kufariki wakati wa mwezi wao wa kwanza ikilinganishwa na katika nchi za kipato cha juu.

Mwaka 2018 mmoja ya watoto 13 katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara walikufa kabla ya mwaka wao wa tano ikiwa hii ni mara 15 zaidi juu, kuliko ile hatari inayowakumba watoto barani Ulaya ambapo ni j mmoja tu kati ya wato 196 walio chini ya miaka 5 hufariki.

Wanawake katika nchi za kusini kwa jangwa la sahara hukumbwa na hatari ya 1 kwa 37 kufariki wakati wa ujauzito au wakati wa kujifungua ambapo hatari ya mwanamke kufariki Ulaya ikiwa ni 1 kwa 6500. Kusini mwa jangwa la sahara na kusini mwa Asia huchukua asilimia 80 ya vifo vya akina mama na watoto duniani.

Hatua zilizopigwa

Dunia imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya watoto na akina mama. Tangu mwaka 1990, kuna kupungua kwa asilimia 56 ya vifo vya watoto walio chini ya miaka 15 kutoka milioni 14.2 hadi milioni 6.2 mwaka 2018.

Nchi zilizo mashariki na kusini mashariki mwa Asia zimepiga hatua kubwa zaidi zikiwa na kupungua kwa asilimia 80 ya watoto walio chini miaka mitano.

Na kuanzia mwaka 2000 hadi 2017 vifo vilipungua kwa asilimia 38 katikati na kusini mwa Asia.

Belarus, Bangladesh, Cambodia, Kazakhstan, Malawi, Morocco, Mongolia, Rwanda, Timor-Leste na Zambia ni baadhi ya nchi ambazo zimeonyesha hatua kubwa katika kupunguza vifo vya watoto na kina mama.