Umoja wa Mataifa wataka kujengwa miundumbinu ya kudumu ili kuokoa maisha na kupunguza watu kuhama

18 Septemba 2019

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kupunguza athari za majanga, Mami Mazutori, hii leo ametoa wito wa kuwepo malengo makubwa katika sekta ya ujenzi kuhakikisha kuwa miundombinu muhimu itastahimili athari za majanga ya mazingira ambayo yamesababisha watu milioni 7 kuhama mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi, Bi. Mazutori amesema kuna ushahidi ulio wazi kuwa mahitaji ya kibinadamu  yanayochochewa na majanga ya mabadiliko ya tabianchi ni makubwa kuliko uwezo wa jamii ya  watoa misaada kuweza kuitikia mahitaji yote.

Amesema kuwa takriban dola trilioni 90 zitawekezwa katika miundombinu ifikapo mwaka 2030 akisema kuwa, ikiwa wataweka miundombinu ya kudumu itakuwa fursa kubwa kuzuia athari mpya za majanga, itaongeza uwezekano wa kumaliza umaskini kwenye nchi za kipato cha chini na cha wastani kwa kupunguza hasara za kiuchumi.

Bi Mizutori amesema kuwa tayari mwaka huu watu wengi wamepoteza maisha na uharibifu wa mali umeshuhudiwa kutokana na majanga ya hali ya hewa kote duniani kuanzia Bahamas hadi Msumbuji, India na Bangladesh akiongeza kuwa athari za majanga ya asili huwa mabaya kutokana na ukosefu wa umakini wakati wa ujenzi.

Amesisitiza kuwa ni lazima kujenga kitu cha kudumu, ikimaanisha kuelewa athari kwa undani zaidi kuliko awali ili kuwaza kuishi kulingana na athari za gesi chafu katika mifumo ya hali ya hewa duniani.

Hii inachangia katokea mawimbi hatari, mafuriko, viwango vya juu vya joto na umaskini na njaa inayosababisha na ukame, aliongeza Bi Mizutori.

Siku ya Kimataifa ya kukabiliana na majanga inaadhimishwa kila mwaka tarehe 13 mwezi Oktoba na mwaka huu kauli mbiu ya mwaka huu kujenga kitu cha kudumu.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud