Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati ni sasa kila nchi kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:UN

Baadhi ya wakulima nchini Malawi wameanza kulima nyanya katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
UNDP Malawi
Baadhi ya wakulima nchini Malawi wameanza kulima nyanya katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Wakati ni sasa kila nchi kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:UN

Tabianchi na mazingira

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesema wakati wa kuchapuza kuchukua hatua zinazohitajika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika ngazi ya taifa ni sasa. Akizungumza na waandishi wa Habari hii leo mjini New York Marekani kuhusu mkutano wa ngazi ya juu dhidi ya mabadiliko ya utakaofanyika wiki ijayo Bi. Mohammed amesema “Tunahitaji kusukuma mbele safari yetu kwa kutumia gia kubwa endapo tunataka kufikia malengo ambayo yamewekwa bayana na sayansi kuhusu mabadiliko ya tabianchi na malengo ya maendeleo endelevu SDGs.”

Naibu Katibu Mkuu amewaeleza waandishi wa Habari mtazamo wa mikakati ambayo inaweza kutarajiwa kutoka kwenye mkutano huo wa ngazi ya juu wa hatua dhidi ya tabianchi. “Mkutano huo utawasilisha hatua mpya ambazo zinatekelezeka ambazo mosi zitaharakisha mchakato wa kuhama kutoka kwenye matumizi ya makaa ya mawe na kuingia katika nishati safi na salama na kupunguza kiwango cha uchafuzi wa hali ya hewa ambao unaathiri afya zetu.”

Mkakati wa pili amesema ni “kulinda mazingira ikiwemo maliasili , lakini pia kutambua uwezo wa maliasili kutupa suluhu dhidi ta mabadiliko ya tabianchi “. Tatu ameongeza kuwa ni “kuunda njia ambazo ni salama, zinazojali mazingira ambazo zitafanya kazi na kusongesha kwa kasi mabadiliko na sekta muhimu kutoka uchumi unaoharibu mazingira kwenda kwenye uchumi unaojali mazingira kwa lengo la kuwalinda watu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo tayari zinashuhudiwa hivi sasa na kuhakikisha kwamba hakuna anayesalia nyuma.”

Kuhusu masuala ya uzalishaji wa makaa ya mawe Bi. Mohammed amesema “Tunajua kwamba kuachana na masuala ya makaa ya mawe si mchakato rahisi ambao utamfaa kila mtu, ni suala tata. Katika baadhi ya nchi nishati adidifu gharama zake tayariu ni nafuu kuliko makaa ya mawe ba nchgakato wa mabadiliko unaendelea. Katika nchi nyingine mabadiliko hayo yanahitaji msaada zaidi na hususan ufadhili kwa ajili ya nishati adidifu.”

Amesisitiza kuwa “Haitoshi tu kuacha kufadhili makaa ya mawe bali  ufadhili ni lazima uhamishiwe katika kuwezesha nishati adidifu. Hivyo kuna haja ya kuangalia kwa makini na kuelekeza mguvu zetu katika hilo.”

Naye mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkutano wa ngazi ya juu wa hatua za mbadiliko dhidi ya tabianchi Luis Alfonso de Alba alipoulizwa kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika mkutano utakaofanyika jumamosi wa vijana amesema “Vijana wanatoa mapendekezo kwa nchi wanachama na wadau wengine na pia watatayatrisha mikakati kadhaa wao wenyewe  ya mambo ambayo wanaahidi kuyafanya.Na hayo yote yanawekwa bayana mwishoni mwa wiki na pia yatawasilishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano.”

Tarehe 23 Septemba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atakuwa mwenyeji wa mkutano wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika katika makao makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani kwa lengo la kupiga jeki na kusongesha kwa kasi utekelezaji wa mkataba wa Paris. Katibu Mkuu analenga kuonyesha jitihada za pamoja na katika ngazi ya taifa na utashi wa kisiasa  katika utekelezaji huo , kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuingia katika uchumi unaojali mustakabali wa dunia hii na watu wake.

Mkutano wa vijana kuhusu tabianchi ni jukwaa  kwa ajili ya viongozi vijana ambao wanasongeshja hatua  dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuwasilisha suluhu zao kwenye Umoja wa Mataifa na pia kupata fursha ya kujihusisha na wafanya maamuzi katika kutathimini na kujadili masuala yanayotoa changamoto katika zama hizo.