Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi

Kituo cha kawi kutokana na nishati ya jua.
World Bank/Dana Smillie
Kituo cha kawi kutokana na nishati ya jua.

Mabadiliko ya tabianchi

Tabianchi na mazingira

Umoja wa Mataifa unajitayarisha kwa ajili mkutano wa “Kuchukua Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi Septemba mwaka wa 2019 huko New York, Marekani ambao ni moja ya mikutano ya ngazi ya juu ya tabianchi katika siku za karibuni, cha kujiuliza nihatua gani ambayo ulimwengu umepiga katika kukabiliana na shida ya tabianchi, na maendeleo hayo yanapimwaje?

Karibu miaka mitatu iliyopita, jamii ya kimataifa ilikusanyika huko Paris Ufaransa ili kuweka mkakati wa pamoja wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Walikubaliana kufanya juhudi kuzuia ongezeko la joto duniani na kuhakikisha linakuwa "chini ya" nyuzi joto 2  zaidi ya viwango vya awali vya kabla ya maendeleo ya viwanda na, ikiwa inawezekana, kufikia nyuzi joto 1.5.

Walakini, Julai mwaka huu wa 2019 hali ya joto ilipundukia  nyuzi 1.2  zaidi ya viwango hivyo na hata kuvunja, rekodi ya mwezi uliokuwa na joto zaidi tangu kuanza kuorodheshwa kwa rekodi za joto kali Zaidi duniani. Hii inamaanisha dunia imeweza kurekodi miaka mitano yenye joto zaidi kwenye katika historia, kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres.

Bwana Guterres amesema “tuko katika mashindano yanayokwenda kwa kasi sana kuliko kasi tuliyonayo ya kupmbana na mabadiliko ya tabianchi n ani mbio ambazo lazima tushinde”. Habari za Umoja wa Mataifa zinatathimini kwa karibu moja ya vyombo muhimu vya kimataifa vinavyotumika kufuatilia vita hivi dhidi ya ongezeko la joto ulimwenguni na mchango wa kila nchi, au NDCs.

 NDC ni nini?

Inapaswa kuelekweka kwamba mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi haufungi kisheria na wala hauziambii nchi jinsi zinavyopaswa kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi kudhibiti mabadiliko ya tabianchi , lakini inazihimiza nchi kujikatia tiketi zao wenyewe.

Mipango hii ya tabianchi inaelezea ni nini nchi inaahidi kufanya, na ni kiasi gani wanapanga kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. Kwa ktambua kwamba nchi zinazoendelea mara nyingi hazina rasilimali, fedha, na teknolojia, Mkataba wa Paris unatoa wito kwa nchi zinazoendelea kuonyesha kile zinachoweza kufanya peke yao, na nini wanachoweza kufanya kwa msaada kutoka kwa jamii ya kimataifa.

Kwa nini ni muhimu?

Nchi zina njia nyingi za kuchagua jinsi zinavyoweza kufuata malengo ya Mkataba wa Paris. Hii inaweza kuhusisha sheria, motisha za kifedha, au sera za ushuru kukuza shughuli ambazo zitapunguza uzalishajiw wa gesi chafuzi. Kwa mfano, nchi zinaweza kuamua kuweka bei kwenye hewa ukaa , kupitia ushuru au kwa kujenga mfumo wa biashara ya hewa ukaa.

Lengo ni kwamba, endapo watu watafahamu vyema gharama ya uchafuzi utokanao na hewa ukaa watawekeza katika maeneo, au mafuta, ambayo yanagharimu kidogo. Kwa raia wa Maisha ya kkawaida hii inaweza kuathiri aina ya magari, au viyoyozi,  au mfumo wa baridi wanaotumia, katika Nyanja mbalimbali za Maisha yao.

Zaidi ya hayo, sera hizi zinaweza kusaidia kudhibiti maendeleo katika maeneo ambayo yako hatarini zaidi kwa athari za mabadiliko ya tabianchi, kama maeneo ya mwambao ambayo yanakabiliwa na changamoto ya kuongezeka kwa kina cha bahari

Hifadhi ya kuzalisha nishati ya upepo nje kidogo ya mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott. (11 Januari mwaka wa 2019), na UNDP Mauritania / Freya Morales

Kituo kinachoendeshwa na nguvu ya upepo kwenye mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott.(Januari 11 2019)
UNDP Mauritania/Freya Morales
Kituo kinachoendeshwa na nguvu ya upepo kwenye mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott.(Januari 11 2019)

 Kwa nini tunajadili haya sasa?

Kwa mujibu wa mkataba wa Paris, nchi zinastahili kuongeza juhudi za mchango wao kila baada ya miaka michache ili ari yao ya utekelezaji.

Hii inajulikana kama utaratibu wa "ratchet", ikimaanisha kwamba uwasilishwaji wa sio ukomo wa malengo yao ya awali na haujafikia ambapo tunahitaji kuwa: hata ikiwa ungeongeza NDCs za nchi zote, bado tutakuwa tutakuwa tu robo tatu ya ya tunapohitaji kuwa, ili kufikia Malengo ya Paris.

Kwa hivyo, nchi zinapaswa kupeleka tathimini zilizosasishwa na kuboreshwa mwaka wa 2020, na ni muhimu kuchagiza  sasa, ili kushinikiza kwa kiasi kikubwa kuchukua hatua: hii ndio sababu Mkutano wa kuchukua Hatua dhidi yamabadiliko ya tabianchi unafanyika mnamo Septemba mwaka huu wa 2019.

Je yote ni zahma na kiza?

La hasha! Tunaona ongezeko la hatua zinazochukuliwa ulimwenguni kote watu kuhamia kwenye nishati mbadala, mitambo mikubwa ya umeme wa jua ikijengwa huko Moroco na Falme za Kiarabu, huku Ureno ikipokea nishati yake kutoa kwa nishati jadidifu na nchi nyingi zimegundua kuwa  zinaweza kupata nishati yake  kwa kutumia nishati mbadala.

Uwekezaji katika nishati mbadala sasa unaongoza kuliko hata wa sekta ya mafuta, haswa katika nchi zinazoendelea, na nchi nyingi zikiwemo ndogo zimefanikiwa kupunguza athari za hewa ukaa

Wakati huo huo, ukweli ni kwamba dunia haiendi kwa kasi ya kutosha: uchafuzi wa hali ya hewa unaongezeka na joto nalo linaongezeka.

Majengo huko Jamhuri ya Dominica yakikarabatiwa au kujengwa upya baada ya kisiwa hicho kuharibiwa na kimbunga Irma. (16 Februari mwaka wa 2018), UNDP / Zaimis Olmos

Mijengo Dominica zinakarabatiwa baada ya kisiwa hicho kuharibiwa na kimbunga Irma. (Februari 16 2018)
UNDP/Zaimis Olmos
Mijengo Dominica zinakarabatiwa baada ya kisiwa hicho kuharibiwa na kimbunga Irma. (Februari 16 2018)

Ni kanda gani inayoongoza njia?

Hakuna kanda inayozidi nyingine, lakini kuna nchi, na miji, ambayo inaonyesha maendeleo makubwa. Nchi nyingi, pamoja na Visiwa vidogo vinavyoendelea, na Kisiwa cha Pasifiki, zimesema kwamba zinaelekea kwenye hali ya kudhibi mabadiliko ya tabianchi na kutokubali kabisa kuwa na alama isiyofutika ya hewa ukaa.

Kwa vitendo hii inamaanisha kwamba wameweza kuweka uiwano katika kudhibiti kuzalisha hewa ukaa , kwa mfano katika viwanda na hata katika matumizi ya gari tu kuondolewa kwa kiasi kikubwa kwa hewa chafuzi ya ukaa angani kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kupanda miti zaidi ambayo inanyonya hewa ukaa.

Ni jambo la kusikitisha kwamba nchi hizi, kati ya zilizoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi, zimechangia kidogo sana katika tatizo hilo.

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi zinahitaji uwekezaji, na hiyo mara nyingi kunahitajika sera nzuri za serikali ili kutoa motisha. Pamoja na Ureno, nchi zingine kadhaa zimewekeza sana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi zikiwemo  Chile, Ireland, Kenya na Costa Rica na mataifa mengi ya Ulaya yamepiga gatua kubwa katika katika kupunguza uzalishaji wao wa hewa chafuzi.

Je tutawezaje kupiga hatua kwa kasi?

Tunahitaji kuona uongozi bora wa kisiasa na utashi wa kisiasa. Kuendelea na maisha kama kawaida itakuwa itakuwa ni kosa kubwa na itasababisha kuongezeka kwa joto ulimwenguni kwa nyuzi joto tatu, au zaidi, katika karne hii.

Uongozi imara, kwa upande wa serikali, wafanyibiashara na viongozi wa asasi za kiraia, ni muhimu kwa kuendeleza hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Watu huleta mabadiliko pia: Mabadiliko ya tabia za watumiaji bidhaa  ni muhimu katika kufikia uchumi usio na hewa ukaa nyingi, ndiyo maana Umoja wa Mataifa umeendeleza Kampeni ya kuchukua hatua sasa au ActNow, ili kutoa maoni ya msingi ya hatua ambazo sisi sote tunaweza kuchukua.

Hivyo tunaweza kutatua janga la mabadiliko ya tabianchi?

Ndio. Tunazo suluhu ambazo tunaweza kuzitumia kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, lakini tunahitaji kuzitumia suluhu hizo

Tunahitaji kuhamisha uwekezaji kutoka kwenye uchumi “mchafu” ili kwenda kwenye uchumi unaojali mazingira. Fedha zipo, tunayo teknolojia sasa tunahitaji kuifanya iweze kuwafikia watu wote  katika nchi zote.

Lakini tunahitaji kuchukua hatua sasa. Kila kiasi cha ongezeko la joto kizingatiwe, na tunavyoendelea kusubiri kwa muda mrefu, athari mbaya nazo zinazidi kuongezeka.